-
Ala za Muziki Katika Israeli la KaleAmkeni!—2011 | Machi
-
-
Matari, Matasa, na Matoazi
Baada ya Mungu kumwongoza Musa pamoja na wana wa Israeli kimuujiza kupitia Bahari Nyekundu, Miriamu, dada ya Musa, pamoja na “wanawake wote,” walitoka “wakiwa na matari na kucheza dansi.” (Kutoka 15:20) Ingawa matari yaliyotumiwa wakati wa Biblia hayajachimbuliwa, sanamu za udongo zenye umbo la mwanamke akiwa ameshika ngoma ndogo zimepatikana huko Israeli katika sehemu mbalimbali kama vile Akzibu, Megido, na Beth-sheani. Huenda ala hiyo inayoitwa tari katika tafsiri za Biblia, ilikuwa kama pete kubwa ya mbao na ilifunikwa kwa ngozi upande mmoja.
Katika nyakati za wazee wa ukoo, matari yalichezwa na wanawake walioimba na kucheza dansi wakati wa sherehe. Biblia inaeleza kwamba wakati Yeftha, kiongozi wa Israeli aliporudi nyumbani baada ya kushinda pigano muhimu, binti yake alitoka nje kumpokea huku “akipiga tari na kucheza dansi.” Katika pindi nyingine, wanawake walisherehekea ushindi wa Daudi “wakiimba na kucheza dansi” “wakiwa na matari.”—Waamuzi 11:34; 1 Samweli 18:6, 7.
-
-
Ala za Muziki Katika Israeli la KaleAmkeni!—2011 | Machi
-
-
[Picha katika ukurasa wa 15]
Tari limetumiwa tangu nyakati za wazee wa ukoo
-