-
Ala za Muziki Katika Israeli la KaleAmkeni!—2011 | Machi
-
-
Tarumbeta na Baragumu
Mungu alimwagiza Musa atengeneze tarumbeta mbili. Zilitengenezwa kwa kutumia fedha iliyofuliwa, au kupigwa. (Hesabu 10:2) Makuhani walizipiga wakitangaza matukio mengi yaliyohusu hekalu pamoja na sherehe mbalimbali. Sauti tofauti zilipigwa ikitegemea kusudi la tukio, kama vile sauti ya juu sana iliyopigwa kwa muda mrefu au kwa muda mfupi. Umbo halisi la tarumbeta hizo halijulikani kwa sababu hakuna tarumbeta zozote za nyakati za Biblia ambazo zimechimbuliwa. Ni michoro ya wasanii pekee ambayo inapatikana, kama ule unaopatikana kwenye Tao la Tito huko Roma.
-
-
Ala za Muziki Katika Israeli la KaleAmkeni!—2011 | Machi
-
-
[Picha katika ukurasa wa 15]
Tarumbeta ilitumika kutangaza matukio mengi
-