Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Unabii wa Biblia Unasema Chochote Kuhusu Kuanzishwa kwa Taifa la Israeli la Kisasa?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Novemba 1
    • Ulimwengu pia ulitazama Mashariki ya Kati kwa wasiwasi mnamo Mei 1948. Wakati huo, miaka 62 iliyopita, mamlaka ya Uingereza ya kusimamia maeneo ambayo wakati huo yaliitwa Palestina ilikuwa inakaribia kuisha, na vita vilikuwa karibu kuanza. Mwaka uliotangulia, Umoja wa Mataifa ulikuwa umetoa kibali cha kuanzishwa kwa Taifa huru la Wayahudi katika sehemu fulani ya maeneo hayo yaliyosimamiwa na Uingereza. Mataifa jirani ya Waarabu yalikuwa yameapa kufanya chochote kile ili kuzuia kuanzishwa kwa taifa hilo. “Mpaka wetu na taifa hilo utakuwa moto na damu,” ukaonya Ushirika wa Nchi za Kiarabu.

      Ilikuwa Ijumaa saa 10:00 alasiri, Mei 14, 1948, na baada ya saa chache tu, mamlaka ya Uingereza ya kusimamia Palestina ingefikia mwisho. Kwenye Jumba la Makumbusho la Tel Aviv, kikundi cha watazamaji 350 waliokuwa wamefika baada ya kualikwa kisiri, walingoja kwa hamu kutangazwa rasmi kwa taifa la kisasa la Israeli. Kulikuwa na ulinzi mkali ili kuhakikisha kwamba maadui wa Taifa hilo jipya hawavurugi tukio hilo.

      David Ben-Gurion, kiongozi wa Baraza la Taifa la Israeli, alisoma tangazo la kuundwa kwa Taifa la Israeli (The Declaration of the Establishment of the State of Israel). Tangazo hilo lilisema hivi kwa sehemu: “Sisi, washiriki wa Baraza la Watu, wawakilishi wa Jumuiya ya Nchi ya Israeli . . . kwa msingi wa haki yetu ya kiasili na ya kihistoria na kwa msingi wa Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, tunatangaza kuanzishwa kwa Taifa la Wayahudi katika nchi ya Israeli, ambalo litaitwa Taifa la Israeli.”

  • Je, Unabii wa Biblia Unasema Chochote Kuhusu Kuanzishwa kwa Taifa la Israeli la Kisasa?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Novemba 1
    • [Picha katika ukurasa wa 27]

      David Ben-Gurion, Mei 14, 1948

      [Hisani]

      Israel Government Press Office, Photographer: Kluger Zoltan

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki