Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Yoeli na cha Amosi
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Oktoba 1
    • Pia katika siku za Uzia, Amosi, mkaaji wa Yuda ambaye alikuwa “mchungaji na mminyaji wa tini za mikuyu,” anapewa utume wa kuwa nabii. (Amosi 7:14) Tofauti na Yoeli, ambaye anatoa unabii huko Yuda, Amosi anatumwa kaskazini kwenye ufalme wa makabila kumi ya Israeli. Kitabu cha Amosi ambacho kilikamilika karibu mwaka wa 804 K.W.K. baada ya nabii huyo kurudi Yuda, kimeandikwa kwa lugha rahisi lakini yenye kuvutia.

  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Yoeli na cha Amosi
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Oktoba 1
    • Namna gani ufalme wa Israeli wa makabila kumi? Dhambi zake zinatia ndani kuwakandamiza maskini kwa pupa, mwenendo mpotovu kiadili, na kuwatendea kwa dharau manabii wa Yehova. Amosi anaonya kwamba Yehova ‘atatoza hesabu madhabahu za Betheli’ na ‘kuiangusha nyumba ya wakati wa majira ya baridi kali pamoja na nyumba ya wakati wa kiangazi.’—Amosi 3:14, 15.

      Ingawa tayari wameadhibiwa kwa njia mbalimbali, Waisraeli wanaoabudu sanamu wanaendelea kuwa na shingo ngumu. Amosi anawaambia hivi: “Jitayarishe kukutana na Mungu wako.” (Amosi 4:12) Kwa Waisraeli, siku ya Yehova itamaanisha kupelekwa “uhamishoni ng’ambo ya Damasko,” yaani, Ashuru. (Amosi 5:27) Amosi anakabili upinzani kutoka kwa kuhani wa Betheli lakini haogopeshwi kamwe. “Mwisho umewafikia watu wangu Israeli,” Yehova anamwambia Amosi. “Sitawasamehe zaidi tena.” (Amosi 8:2) Wala Kaburi wala milima iliyoinuka haiwezi kuwazuia wasipate hukumu za Mungu. (Amosi 9:2, 3) Lakini kuna ahadi ya kurudishwa. “Nitakusanya na kurudisha mateka wa watu wangu Israeli, nao watajenga majiji yaliyofanywa ukiwa na kukaa ndani yake, watapanda mashamba ya mizabibu na kunywa divai yake, watafanyiza bustani na kula matunda yake.”—Amosi 9:14.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki