-
Yehova Huwavuta Wanyenyekevu Kuijua KweliMnara wa Mlinzi—2003 | Oktoba 1
-
-
Mapema mwaka wa 1949, mwanamume mmoja mrefu mwenye urafiki aliitembelea familia ya Koda. Aliitwa Donald Haslett, naye alikuwa amekuja Kobe kutoka Tokyo ili kutafutia mishonari nyumba. Yeye alikuwa mishonari wa kwanza kabisa wa Mashahidi wa Yehova kuja Japani. Alipata nyumba, na mnamo Novemba 1949, mishonari kadhaa wakaja Kobe.
-
-
Yehova Huwavuta Wanyenyekevu Kuijua KweliMnara wa Mlinzi—2003 | Oktoba 1
-
-
Kuanzia Desemba 30, 1949, mpaka Januari 1, 1950, kusanyiko la kwanza nchini Japani lilifanywa kwenye makao ya mishonari ya Kobe. Nilienda huko pamoja na Maud. Ukiwa kwenye nyumba hiyo kubwa iliyokuwa ya askari mmoja wa Nazi, ungeweza kuona vizuri Kisiwa cha Awaji na Bahari Iliyo Katikati ya Visiwa.
-