-
Nilisaidiwa Kuacha Kuwa Mwenye HayaMnara wa Mlinzi—2000 | Juni 1
-
-
Wakati uo huo, ofisi ya zamani ya tawi iliyokuwa katikati ya Tokyo ilirekebishwa. Baadaye, ikawa makao ya mishonari kwa zaidi ya mishonari 20 ambao wametumikia nchini Japani kwa miaka 40 au 50 au zaidi, kutia ndani mimi na mwenzangu wa muda mrefu, Martha Hess. Daktari mmoja na mke wake, ambaye ni mwuguzi, pia wanaishi katika makao yetu. Wao hututunza, wakishughulikia kwa upendo mahitaji yetu ya kiafya. Hivi karibuni, mwuguzi mwingine amejiunga nasi na dada Wakristo huja kuwasaidia wauguzi hao wakati wa mchana. Washiriki wawili wa familia ya Betheli ya Ebina huja kwa zamu kututayarishia mlo na kusafisha makao yetu. Kwa kweli Yehova amekuwa mwema kwetu.—Zaburi 34:8, 10.
-
-
Nilisaidiwa Kuacha Kuwa Mwenye HayaMnara wa Mlinzi—2000 | Juni 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 24]
Kulia: Washiriki wa makao yetu ya mishonari ya Tokyo
-