-
Nilisaidiwa Kuacha Kuwa Mwenye HayaMnara wa Mlinzi—2000 | Juni 1
-
-
Punde tu baada ya mkusanyiko wa kimataifa wa 1958 uliofanyiwa Yankee Stadium na Uwanja wa Polo huko New York City, tulifunga safari ya kwenda Tokyo kwa meli. Tulikumbwa na kimbunga tulipokaribia bandari ya Yokohama, ambako tulilakiwa na Don na Mabel Haslett, Lloyd na Melba Barry, na mishonari wengine. Wakati huo, kulikuwa na Mashahidi 1,124 pekee nchini Japani.
-
-
Nilisaidiwa Kuacha Kuwa Mwenye HayaMnara wa Mlinzi—2000 | Juni 1
-
-
Na si mimi tu ambaye nimeweza kufanya hivyo, lakini nimeona mamia, hata maelfu, ya wengine pia wakifanya hivyo. Na wamefanya hivyo kwa matokeo mazuri sana hivi kwamba wale Mashahidi waliokuwa zaidi tu ya elfu moja nchini Japani nilipofika huko mwaka wa 1958, wamepita 222,000 leo!
Tulipofika na Martha Japani kwa mara ya kwanza, tulipewa mgawo wa kuishi kwenye ofisi ya tawi jijini Tokyo. Mwaka wa 1963, ofisi mpya yenye orofa sita ilijengwa mahali hapo, na tumeishi hapo tangu wakati huo hadi sasa. Mnamo Novemba 1963 tulikuwa miongoni mwa wale 163 waliosikiliza hotuba ya kuweka wakfu iliyotolewa na msimamizi wa tawi, Lloyd Barry. Kufikia wakati huo tulikuwa Mashahidi 3,000 nchini Japani.
Imependeza sana kuona kazi ya kuhubiri juu ya Ufalme ikikua haraka sana, tukifikia zaidi ya Mashahidi 14,000 mwaka wa 1972 wakati ambapo ofisi mpya ya tawi iliyoongezwa ilimalizika katika jiji la Numazu. Lakini, kufikia mwaka wa 1982 kulikuwa na watangazaji wa Ufalme zaidi ya 68,000 nchini Japani, na ofisi kubwa zaidi ilijengwa katika jiji la Ebina, kilometa 80 hivi kutoka Tokyo.
-