Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tii Onyo!
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Februari 15
    • Tii Onyo!

      PUU! Mnamo Juni 3, 1991, Mlima Fugen nchini Japani ulilipuka kwa mshindo mkubwa wenye ngurumo ukimwaga gesi na majivu ya volkano. Mchanganyiko huo uliokuwa moto sana ulitiririka chini ya mlima. Mlipuko huo ulisababisha vifo vya watu 43. Wengi walioponea chupuchupu walikuwa wamechomeka vibaya. “Maji, maji, tafadhali,” wengine wakalia. Zimamoto na polisi wakaenda mbio sana kuwasaidia.

      MAWE yaliyoyeyuka yalikuwa yameonekana kwenye kilele cha Mlima Fugen majuma mawili hivi awali, kwa hiyo wenye mamlaka na wakazi walikuwa macho. Kwa muda wa zaidi ya juma moja kabla ya msiba huo, watu walikuwa wameshauriwa waondoke kwenye eneo hilo. Siku moja tu kabla ya mlipuko huo, polisi walikuwa wamewaomba waandishi wa habari wasiingie katika eneo hilo marufuku. Lakini, alasiri hiyo yenye msiba watu 43 walikufa katika eneo hilo la hatari.

      Kwa nini watu wengi hivyo walijasiria kuingia katika eneo hilo au kubaki humo? Wakulima fulani waliokuwa wamehama nyumba zao walirudi kutazama mali zao na mashamba yao. Wataalamu watatu wa mambo ya volkano walikuwa wakijaribu kuikaribia volkano hiyo kwa kadiri iwezekanavyo ili waridhishe tamaa yao ya kitaaluma. Waandishi kadhaa wa habari na wapiga-picha walithubutu kuvuka mpaka wa eneo marufuku kwa sababu walitaka kutoa habari motomoto juu ya mlipuko huo. Madereva watatu wa teksi zilizokuwa zimekodishwa na waandishi wa habari walikuwa katika eneo hilo. Polisi na zimamoto wa kujitolea walikuwa kazini. Kila mmoja wao alikuwa na sababu yake ya kuingia katika eneo la hatari—na matokeo yakawa kifo.

  • Epuka Eneo la Hatari!
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Februari 15
    • NI WAJIBU wa wataalamu wa mambo ya volkano kuchunguza na kuchanganua ishara kisha kuonya watu juu ya milipuko ya volkano inayokaribia. (Mlima Fugen ulipolipuka, polisi walilazimika kuzuia watu wasiingie kwenye eneo la hatari.)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki