-
Epuka Eneo la Hatari!Mnara wa Mlinzi—2000 | Februari 15
-
-
Kama ilivyokuwa na mlipuko wa Mlima Fugen, tunahitaji kuchukua hatua kuhusiana na onyo hilo. Kumbuka kwamba waandishi wa habari na wapiga-picha angalau 15 waliotaka kupata habari motomoto walikufa. Kwa kweli, mpiga-picha mmoja alikufa kidole chake kikiwa kwenye kidude cha kupigia picha. Mtaalamu mmoja wa mambo ya volkano—ambaye alikuwa amesema, “Ikiwa siku moja nitakufa, nataka nife karibu na volkano”—alikufa tu kama alivyotaka. Wote walikuwa wamejitoa kwa kazi yao na shughuli zao. Lakini walikufa—matokeo ya kupuuza onyo.
-
-
Epuka Eneo la Hatari!Mnara wa Mlinzi—2000 | Februari 15
-
-
Kwenye Mlima Fugen, zaidi ya polisi 12 na zimamoto wa kujitolea walikuwa kazini wakati mtiririko moto sana wa volkano ulipowaua. Walikuwa wakijaribu kuwasaidia na kuwalinda watu waliokuwa hatarini. Walikuwa kama wanaume na wanawake wenye nia njema wanaojihusisha sana na kuboresha mambo katika ulimwengu huu. Ingawa huenda wakawa na nia nzuri, “yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa.” (Mhubiri 1:15) Mfumo wa mambo ambao umepotoka hauwezi kunyoshwa. Je, ni jambo linalopatana na akili kuwa “rafiki wa ulimwengu” kwa kujaribu kuokoa mfumo wa ulimwenguni pote ambao Mungu ameazimia kuuondoa?
-
-
Epuka Eneo la Hatari!Mnara wa Mlinzi—2000 | Februari 15
-
-
Na tusisahau wakulima ambao, baada ya kuhamishwa, walirudi kutazama mashamba yao karibu na Mlima Fugen. Yaelekea walikuwa wakitamani sana kurudia maisha ya “kawaida” waliyokuwa wakiishi. Lakini unatambua kwamba uamuzi wao wa kurudi haukuwa wa hekima. Yamkini hilo halikuwa ndilo jaribio lao la kwanza kuingia katika eneo la hatari. Huenda waliingia katika eneo hilo la hatari kwa muda mfupi tu bila chochote kutukia. Huenda wakati ule mwingine walikaa kwa muda mrefu kidogo, na bado hakuna chochote kilichotukia. Yaelekea sasa walizoea kuvuka mpaka wa usalama na kupata ujasiri wa kukaa kwa muda mrefu katika eneo la hatari.
-
-
Epuka Eneo la Hatari!Mnara wa Mlinzi—2000 | Februari 15
-
-
Pia, fikiria wale madereva watatu wa teksi ambao walikufa wakingojea waandishi wa habari na wapiga-picha wakati mtiririko wa volkano ulipotiririka kwa kasi chini ya mlima. Leo wengine wanaweza kuandamana na watu ambao wamejasiria kurudi katika ulimwengu. Hata sababu iwe nini, ni wazi kwamba haifai kujihatarisha kwa kushawishwa urudi katika eneo la hatari.
Wote waliokufa kutokana na mlipuko wa Mlima Fugen walivuka mpaka wa usalama na kuingia katika eneo la hatari. Ingawa walitarajia kwamba mlima huo ungelipuka siku moja, hakuna hata mmoja aliyefikiri ungelipuka siku hiyo. Kwa kuchunguza ishara ya umalizio wa mfumo wa mambo, wengi wanatarajia siku ya Yehova ije wakati fulani lakini yaelekea hawaitarajii ije karibuni. Wengine hata wanaona kwamba siku hiyo haiwezi kuwa “leo.” Mtazamo kama huo ni hatari kwelikweli.
-