Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Mungu Ana Watu Wanaomtumikia kwa Utaratibu?
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Juni 1
    • Israeli la Kale—Taifa Lenye Utaratibu Mzuri

      Yehova Mungu alimtumia Musa kuhakikisha kwamba Waisraeli wanafanya ibada ya kweli kwa utaratibu mzuri. Fikiria mipango ya kupiga kambi walipokuwa katika nyika ya Sinai. Bila shaka, kungekuwa na mvurugo kama kila familia ingeruhusiwa kupiga kambi popote ilipochagua. Yehova aliwapa Waisraeli maagizo hususa kuhusiana na mahali ambapo kila kabila lingepaswa kupiga kambi. (Hesabu 2:1-34) Sheria ya Musa pia ilikuwa na maagizo hususa kuhusu afya na usafi—kwa mfano, kuhusu kuondoa kinyesi cha binadamu.—Kumbukumbu la Torati 23:12, 13.

      Waisraeli walipoingia katika Nchi ya Ahadi, walikuwa taifa lenye utaratibu mzuri katika njia nyingi. Taifa hilo liligawanywa katika makabila 12 na kila kabila likagawiwa sehemu yake ya ardhi. Sheria ambayo Yehova alitoa kwa taifa hilo kupitia Musa ilihusu kila sehemu ya maisha ya Waisraeli—ibada, ndoa, familia, elimu, biashara, chakula, kilimo, ufugaji, na kadhalika.b Ingawa sheria nyingine zilieleza mambo waziwazi na kwa undani, zote zilikuwa wonyesho wa jinsi Yehova alivyowajali watu wake. Pia, zilichangia furaha miongoni mwao. Kwa kufuata mipango hiyo yenye upendo, Waisraeli walifurahia uhusiano wa pekee pamoja na Mungu.—Zaburi 147:19, 20.

      Ingawa ni kweli kwamba Musa alikuwa kiongozi stadi, kufaulu au kutofaulu kwake kulitegemea ushikamanifu wake kwa utaratibu na mwongozo ambao Mungu alitaka ufuatwe, bali si ustadi wake akiwa kiongozi. Kwa mfano, Musa aliamuaje njia ambayo Waisraeli wangefuata nyikani? Yehova aliwaongoza kwa kutumia nguzo ya wingu mchana, na nguzo ya moto usiku. (Kutoka 13:21, 22) Ingawa Mungu aliwatumia wanadamu, yeye mwenyewe ndiye aliyewapanga na kuwaongoza watu wake. Alifanya vivyo hivyo katika karne ya kwanza.

  • Je, Mungu Ana Watu Wanaomtumikia kwa Utaratibu?
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Juni 1
    • [Picha katika ukurasa wa 13]

      Kambi ya Waisraeli ilipangwa kwa utaratibu mzuri

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki