-
Wakristo Wanaodumisha Msimamo wa Kutokuwamo Katika Siku za MwishoMnara wa Mlinzi—2002 | Novemba 1
-
-
7. Kwa nini Wakristo wa kweli hudumisha msimamo wa kutokuwamo, nao wameonyeshaje hivyo?
7 Kwa kuwa Mashahidi ni watu wa Yehova na pia ni wafuasi wa Yesu na raia wa Ufalme wa Mungu, wamedumisha msimamo wa kutokuwamo katika vita vya mataifa na kimataifa katika karne ya 20 na ya 21. Hawaungi mkono upande wowote wa vita, hawatumii silaha dhidi ya mtu yeyote, na hawaenezi habari zisizo za kweli ili kuendeleza mradi fulani wa kilimwengu. Kwa kudhihirisha imani yao kwa njia ya pekee licha ya upinzani mkali sana, wamefuata kanuni walizoelezwa watawala wa Ujerumani ya Nazi mwaka wa 1934: “Hatupendezwi na mambo ya kisiasa, lakini tumejitoa kabisa kwa ajili ya ufalme wa Mungu chini ya Mfalme wake, Kristo. Hatutamdhuru mtu yeyote. Tungependa kuishi kwa amani na kuwatendea watu wote mema tunapopata fursa.”
-
-
Wakristo Wanaodumisha Msimamo wa Kutokuwamo Katika Siku za MwishoMnara wa Mlinzi—2002 | Novemba 1
-
-
11. Upendo uliopo miongoni mwa Mashahidi wa Yehova umekuwa na matokeo gani juu ya mwenendo wao?
11 Leo, Mashahidi wa Yehova hudhihirisha upendo wao wa kidugu kwa kutimiza maneno ya Isaya 2:4: “Watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.” Kwa sababu ya kufundishwa na Yehova, Wakristo wa kweli wanafurahia amani pamoja naye na pia miongoni mwao wenyewe. (Isaya 54:13) Kwa sababu wanampenda Mungu na ndugu zao, hawawezi kutumia silaha dhidi ya Wakristo wenzao—au mtu mwingine—katika nchi nyingine. Amani na umoja walio nao ni sifa muhimu katika ibada yao, nazo huonyesha kwamba kwa kweli wana roho ya Mungu. (Zaburi 133:1; Mika 2:12; Mathayo 22:37-39; Wakolosai 3:14) Wao hujitahidi ‘kutafuta amani na kuifuatia,’ wakijua kwamba “macho ya BWANA huwaelekea wenye haki.”—Zaburi 34:14, 15.
-