Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 10. Ni kwa ushindi gani yule Mfalme mwenye kushinda amebariki watu wake “katika kutetea na kuthibitisha kisheria habari njema”?

      10 Mfalme wetu mwenye kushinda amebariki pia watu wake wenye bidii kwa kuwaongoza kwenye ushindi mwingi “katika kutetea na kuthibitisha kisheria habari njema” katika mahakama ya sheria na mbele ya watawala. (Wafilipi 1:7; Mathayo 10:18; 24:9, NW) Hiyo imekuwa katika mataifa yote—katika Australia, Ajentina, Kanada, Ugiriki, India, Swazilandi, Swizalandi, Uturuki na mabara mengineyo. Miongoni mwa ushindi mbalimbali 50 wa kisheria waliopata Mashahidi wa Yehova katika Mahakama Kuu Zaidi Sana ya United States umekuwa ule unaohakikishia haki ya kujulisha wazi habari njema “peupe na nyumba kwa nyumba” na kutofanya sherehe za kuabudu sanamu za kizalendo. (Matendo 5:42; 20:20, NW; 1 Wakorintho 10:14) Hivyo, njia imeachwa wazi kwa ajili ya kupanua kazi ya kutoa ushahidi katika tufe lote.

  • Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Katika Miaka ya 1930 na 1940, maadui wenye kujikaza walijaribu kufanya ionekane kwamba huduma ya Mashahidi wa Yehova ilikuwa haramu, yenye uhalifu, au hata yenye kufitini serikali. (Zaburi 94:20) Katika mwaka 1936 pekee, kulikuwako kutiwa mbaroni kulikorekodiwa 1,149 katika United States. Mashahidi walipiga vita ya kesi za kisheria mwendo wote kufikia ile Mahakama Kuu Zaidi Sana, na ufuatao ni baadhi ya ushindi wao mbalimbali wenye kutokeza.

      Katika Mei 3, 1943, Mahakama Kuu Zaidi Sana katika kesi ya Murdock v. Pennsylvania iliamua kwamba Mashahidi hawakuhitaji leseni ili waangushe vitabu kwa pesa. Siku iyo hiyo, ule uamuzi katika kesi ya Martin v. City of Struthers ulishikilia kwamba si kinyume cha sheria kupiga kengele ya mlango wakati wa kushiriki kugawa karatasi na vitu vingine vya kuvumisha habari.

      Katika Juni 14, 1943, Mahakama Kuu Zaidi Sana iliamua katika kesi ya Taylor v. Mississippi kwamba Mashahidi hawakutia moyo utovu wa ushikamanifu kwa serikali kwa kuhubiri kwao. Siku iyo hiyo, katika kesi ya West Virginia State Board of Education v. Barnette, Mahakama hiyo ilishikilia kwamba baraza la shule halikuwa na haki ya kufukuza kutoka shuleni watoto wa Mashahidi wa Yehova waliokataa kusalimu bendera. Kesho yake yenyewe, Mahakama Kuu ya Australia iliyojaa iliondoa marufuku ambayo nchi hiyo iliwekea Mashahidi wa Yehova, hiyo ikitangazwa kuwa “isiyo ya haki, bila sababu nzuri na yenye uonevu.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki