-
“Asanteni kwa Kuwapenda Watu Sana”Amkeni!—2008 | Agosti
-
-
◼ Kilomita 5,500 hivi magharibi ya Chita, mwakilishi wa ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Urusi alikaribishwa kwenye sherehe ya pekee iliyoandaliwa na wasimamizi wa wilaya ya St. Petersburg. Kwa nini? Kila mwaka, baada ya theluji kuyeyuka, Mashahidi wa eneo hilo husaidia kuondoa takataka ambazo zimejikusanya kwenye barabara yenye urefu wa kilomita 60 iliyo karibu na ofisi ya tawi. Ili kuonyesha shukrani kwa roho hiyo ya ushirikiano, ofisa mmoja alimpa mwakilishi wa ofisi ya tawi cheti cha sifa njema. Wahudhuriaji walipiga makofi kwa furaha. Inapendeza kwamba msemaji mmoja katika sherehe hiyo alipotamka vibaya jina la Mungu, Yehova, watu kadhaa ambao si Mashahidi walimsahihisha haraka, wakionyesha kwamba wanafahamu jina la Mungu na watu wanaoitwa kwa jina hilo.
-
-
“Asanteni kwa Kuwapenda Watu Sana”Amkeni!—2008 | Agosti
-
-
[Picha katika ukurasa wa 29]
Ofisi ya tawi ya Urusi ilipata cheti cha sifa njema
-