Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Unapaswa Kuwa Mnyoofu Nyakati Zote?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 1
    • Watu wengi wanaiba kazini. Kwa hiyo, wengi wanasema, “Ikiwa kila mtu anaiba, kwa nini nisiibe?” Hata hivyo, Biblia inasema hivi: “Usiufuate umati kwa ajili ya makusudio maovu.” (Kutoka 23:2) Victoire ametii shauri hilo. Je, amepata matokeo mazuri?

      Alipokuwa na umri wa miaka 19, Victoire alipata kazi katika kiwanda cha kutengeneza mafuta ya mawese. Muda si muda, aligundua kwamba wanawake 40 wanaofanya kazi katika kiwanda hicho walikuwa wakitumia vikapu vyao kuiba mbegu za mafuta hayo na kwenda nazo nyumbani. Kila mwisho-juma, waliuza mbegu hizo na kupata pesa zilizolingana na mshahara wa siku tatu au nne. Victoire anasema hivi: “Kwa kweli, kila mtu alikuwa akifanya hivyo. Walitazamia kwamba nitajiunga nao, lakini nilikataa, na kuwaambia kwamba kuwa mnyoofu ni njia yangu ya maisha. Walinidhihaki, wakidai kwamba ningepata hasara.

      “Siku moja tulipokuwa tukiondoka kwenye kiwanda, meneja alitokea kwa ghafula. Alichunguza kikapu cha kila mtu na kupata mbegu nyingi katika kila kikapu isipokuwa changu. Wote waliopatwa na mbegu hizo waliambiwa kwamba wachague kufutwa kazi papo hapo au kufanya kazi kwa majuma mawili bila mshahara. Katika majuma hayo mawili, wanawake hao waliona wazi kwamba sikupata hasara.”

  • Je, Unapaswa Kuwa Mnyoofu Nyakati Zote?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 1
    • Baada ya muda, Victoire alitoka kwenye kile kiwanda cha kutengeneza mafuta. Alianza biashara yake ya kuuza garri (unga wa mhogo) sokoni. Watu wengi wanapenda kununua unga wake kwa sababu ya unyoofu wake. Baada ya muda, alipunguza muda aliokaa katika soko na kutumia muda zaidi akizungumza na wengine kuhusu tumaini la kuishi katika ulimwengu ambao hautakuwa kamwe na ukosefu wa unyoofu. Baadaye aliolewa, na sasa yeye pamoja na mume wake wanatumika wakiwa wahubiri wa wakati wote.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki