-
Je, Unapaswa Kuwa Mnyoofu Nyakati Zote?Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 1
-
-
Christine ni msimamizi wa shule fulani. Jumatano moja (Siku ya 3) alichukua mshahara wake wa mwezi. Kama watu wengi wanavyofanya huko Afrika Magharibi, alifunga noti hizo pamoja na kuzitia ndani ya mfuko wake. Kisha akapanda pikipiki ya abiria na mara moja akapelekwa kwenye mkutano. Alipofika, alitafuta-tafuta ndani ya mfuko wake sarafu za kumlipa mwendeshaji wa pikipiki. Tayari giza lilikuwa limeingia na bila kujua, pesa alizokuwa nazo zilianguka chini.
Muda mfupi baadaye, Blaise, mwenye umri wa miaka 19, ambaye si mkaaji wa eneo hilo alipitia njia hiyo. Alikuwa amepanga kukutana na rafiki yake kwenye mkutano ambao Christine alikuwa anahudhuria. Aliona bunda la noti akazitia ndani ya mfuko wake. Mkutano ulipokwisha, alimwambia rafiki yake kwamba alikuwa ameokota kitu fulani nje na mtu yeyote aliyepoteza kitu angeweza kumpigia simu na kusema alichopoteza.
Christine alipofika nyumbani jioni hiyo, alishtuka sana kugundua kwamba mshahara wake wa mwezi mzima ulikuwa umepotea. Baada ya juma moja, alipomwambia rafiki yake Josephine, aliambiwa kwamba mgeni fulani aliyehudhuria mkutano alikuwa ameokota kitu fulani. Christine alimpigia simu Blaise na kumwambia kiasi cha pesa alichokuwa amepoteza. Christine alifurahi sana Blaise alipomrudishia pesa hizo. Namna gani Blaise? Alikaa na pesa hizo kwa juma moja, lakini alisema hivi: “Baada ya kurudisha pesa hizo nilipata shangwe nyingi ambayo singepata ikiwa singezirudisha.”
-
-
Je, Unapaswa Kuwa Mnyoofu Nyakati Zote?Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 1
-
-
Christine aliangusha pesa zake mbele ya Jumba la Ufalme la Mashahidi wa Yehova. Blaise hakuwafahamu watu wengi kwenye mkutano huo, lakini alijua kwamba wao ni ndugu na dada zake Wakristo, ambao wanajitahidi kuwa wanyoofu nyakati zote.
-