Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuna Faida za Kuwa Mnyoofu
    Amkeni!—2012 | Januari
    • Faida za Kuaminika

      Unyoofu wako huathiri mafanikio yako​—iwe unajua au hujui. Kisa cha Franz, aliyetajwa katika makala iliyotangulia, kinaonyesha jambo hilo. “Nilipoajiriwa,” anasema, “waajiri wangu walijaribu unyoofu na uaminifu wangu mara kadhaa bila mimi kujua. Nilikuja kujua baadaye kwamba nilipita mtihani huo. Kwa sababu hiyo, nimepewa madaraka zaidi na uhuru zaidi na waajiri wangu wamenithawabisha kwa sababu ya kuwa mnyoofu. Ninajua kwamba kuna watu wanaoweza kufanya kazi yangu kwa njia bora zaidi na walio na akili kuliko mimi. Hata hivyo, nadhani sijafutwa kazi kwa muda wote huu kwa sababu waajiri wangu wananiamini.”

  • Unyoofu Huleta Mafanikio ya Kweli
    Amkeni!—2012 | Januari
    • Kujiheshimu

      “Miaka kadhaa iliyopita, nilimhoji mteja aliyetaka kununua bima ya maisha ambayo ingemgharimu dola milioni moja. Ningelipwa maelfu ya dola kwa kukamilisha mkataba huo. Aliniambia kwamba ili awe mteja wangu, ingebidi nimpe nusu ya pesa nilizopata. Ombi lake lilikuwa kinyume cha maadili na pia tungekuwa tukivunja sheria, nami nilimwambia hivyo waziwazi.

      “Nilijaribu kuzungumza naye na kumwuliza ikiwa angetaka mtu asiye mnyoofu ajue habari zake za kibinafsi na za kifedha ambazo ni siri. Nilimweleza tena msimamo wangu na kumwambia awasiliane nami ikiwa bado angetaka nimwakilishe. Hakuwahi kuwasiliana nami tena.

      “Kama ningekubali ombi lake, ningeacha kuwa mwaminifu na ningeacha kujiheshimu kama Mkristo. Ningekuwa mtumwa wa mwanadamu ambaye alitaka kunishinikiza nijiunge naye katika ukosefu wa unyoofu.”​—Don, Marekani.

      Amani ya Akili

      Kama ilivyotajwa katika makala ya kwanza ya mfululizo huu, mmiliki wa kiwanda fulani alitaka kumpa Danny rushwa kubwa ili adanganye kwamba kiwanda hicho kinaweza kutokeza bidhaa zinazofaa. Danny alifanya nini?

      “Nilimshukuru meneja huyo kwa kunikaribisha kwenye mlo kisha nikamrudishia bahasha hiyo iliyokuwa na pesa. Alinishinikiza kwa kusema kwamba ikiwa kiwanda chake kingepita ukaguzi wetu, angeniongezea pesa zaidi. Nilikataa.

      “Kama ningekubali rushwa hiyo, ningekuwa na wasiwasi daima kwamba nitagunduliwa. Baadaye, mwajiri wangu alipata habari kuhusu kisa hicho. Nilifurahi sana kwamba sikuwa nimefanya jambo lolote lenye ukosefu wa unyoofu. Nilikumbuka andiko la Methali 15:27: ‘Mtu anayepata faida isiyo ya haki anailetea nyumba yake mwenyewe taabu, lakini anayechukia zawadi [au rushwa] ndiye atakayeendelea kuishi.’”​—Danny, Hong Kong.

  • Unyoofu Huleta Mafanikio ya Kweli
    Amkeni!—2012 | Januari
    • Uhusiano Mzuri na Mungu

      “Kazi yangu inahusisha kununua bidhaa kwa ajili ya kampuni yetu. Nyakati nyingine wauzaji huniambia kwamba badala ya kuipunguzia kampuni bei, watanipa kiasi fulani cha faida wanayopata kutoka kwa kampuni yetu. Lakini kufanya hivyo kungekuwa kuiba pesa za kampuni.

      “Mimi hupata mshahara wa chini, na pesa hizo za ziada zingenisaidia sana. Lakini hakuna kitu kinachoweza kulinganishwa na dhamiri safi na kupata kibali machoni pa Yehova Mungu. Kwa hiyo, ninaponunua bidhaa yoyote, mimi hufuata kanuni ya Biblia kwenye Waebrania 13:18: ‘Tunataka kujiendesha kwa unyoofu katika mambo yote.’”​—Raquel, Filipino.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki