-
Yehova Hubariki Ibada SafiUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
15. Ni uzazi gani unaotabiriwa, na unatimizwaje mwaka wa 537 K.W.K.?
15 Hali hiyo ya kurudishwa inaonyeshwa kwa kufaa sana katika mistari ifuatayo ya Isaya: “Kabla hajaona utungu alizaa; kabla maumivu yake hayajampata, alizaa mtoto mwanamume. Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! nchi yaweza kuzaliwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara? Maana Sayuni, mara alipoona utungu, alizaa watoto wake.” (Isaya 66:7, 8) Maneno haya yanatimizwa mara ya kwanza kwa njia ya kusisimua kuhusiana na Wayahudi wahamishwa walioko Babiloni. Sayuni, au Yerusalemu, anaonyeshwa tena kuwa mwanamke anayezaa. Lakini huo ni uzazi wa kushangaza kama nini! Unafanyika upesi sana, ghafula sana, hata kabla ya utungu kuanza! Maelezo ya tukio hilo yanafaa sana. Kuzaliwa kwa watu wa Mungu mwaka wa 537 K.W.K. wakiwa taifa la kipekee kunatukia upesi sana, ghafula sana, hivi kwamba kunaonekana kama mwujiza. Kwani, muda unaopita kuanzia wakati ambao Koreshi anawaweka huru Wayahudi watoke utekwani hadi wakati ambao mabaki waaminifu wanakuwa wamerudia nchi yao, ni miezi michache tu! Hali hiyo inatofautiana kama nini na matukio yaliyotangulia kuzaliwa kwa taifa la Israeli mara ya kwanza! Mwaka wa 537 K.W.K., hakuna haja ya kumwomba mtawala mpinzani atoe uhuru wa kuondoka, hakuna haja ya kukimbia jeshi lenye uadui, hakuna haja ya kukaa-kaa jangwani muda wa miaka 40.
-
-
Yehova Hubariki Ibada SafiUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
17. Yehova anawahakikishiaje watu wake kwamba hakuna cha kumzuia asitimize kusudi lake kuhusiana na Israeli wa kiroho?
17 Katika ulimwengu mzima hakuna nguvu yoyote ambayo ingeweza kuzuia uzaliwa huo mpya. Mstari unaofuata unasema lilo hilo: “Je! mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? asema BWANA; mimi nizalishaye, je! nilifunge tumbo? asema Mungu wako.” (Isaya 66:9) Sawa na vile hatua za kuzaa mtoto zisivyoweza kuepukwa zikiisha kuanza, ndivyo kuzaliwa upya kwa Israeli wa kiroho hakungeweza kuzuiliwa baada ya kuanza. Ni kweli kwamba upinzani ulikuwako, na yaelekea kwamba kutakuwako upinzani zaidi wakati ujao. Lakini ni Yehova peke yake aliye na uwezo wa kukomesha kitu anachokianzisha. Hata hivyo, yeye hafanyi hivyo kamwe! Ingawa hivyo, Yehova anawatendeaje watu wake waliotiwa nguvu mpya?
Utunzaji Mwororo wa Yehova
18, 19. (a) Yehova anatumia mfano gani wenye kugusa moyo, nao unatumikaje kuwahusu watu wake walio uhamishoni? (b) Leo mabaki watiwa-mafuta wamefaidikaje na lishe na utunzaji wenye upendo?
18 Mistari minne inayofuata inaufafanua utunzaji mwororo wa Yehova kwa njia ya kuvutia. Kwanza, Isaya anasema hivi: “Furahini pamoja na Yerusalemu, shangilieni kwa ajili yake, ninyi nyote mmpendao; furahini pamoja naye kwa furaha, ninyi nyote mliao kwa ajili yake; mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa kwa wingi wa utukufu wake.” (Isaya 66:10, 11) Hapa Yehova anatumia mfano wa mwanamke anayenyonyesha kitoto chake kichanga. Mtoto mchanga anapoumwa na njaa, kazi yake ni kulia-lia tu. Lakini anapoletwa karibu na matiti ya mama yake anyonye, sasa yeye huacha kihoro chake na kutosheka akiwa na furaha kamili. Vivyo hivyo, mabaki ya Wayahudi waaminifu walioko Babiloni watatolewa haraka haraka katika hali ya kuomboleza waingie katika hali ya furaha na uradhi ufikapo wakati wao wa kukombolewa na kurudishwa. Watakuwa na shangwe. Yerusalemu litapewa utukufu tena, huku likijengwa upya na kukaliwa upya. Na utukufu wa jiji hilo utaenea uangaze juu ya wakaaji wake wote waaminifu. Kwa mara nyingine, watalishwa kiroho kupitia ukuhani wenye utendaji wa bidii.—Ezekieli 44:15, 23.
-
-
Yehova Hubariki Ibada SafiUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
20. Yerusalemu limebarikiwaje kwa “kijito kifurikacho,” nyakati za kale na za kisasa pia?
20 Unabii unaendelea kusema hivi: “BWANA asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa [“ubavuni,” “NW”]; na juu ya magoti mtabembelezwa.” (Isaya 66:12) Hapa mfano wa kunyonyesha umeunganishwa na wazo la mtiririko wa baraka nyingi, yaani “mto” na “kijito kifurikacho.” Licha ya kubarikiwa kwa amani tele kutoka kwa Yehova, Yerusalemu litabarikiwa pia kwa “utukufu wa mataifa,” unaowatiririkia watu wa Mungu na kuwabariki. Hii inamaanisha kwamba watu wa mataifa watafurika kuwaendea watu wa Yehova. (Hagai 2:7) Katika utimizo wa kale, ni kweli kwamba watu kadhaa wa mataifa mbalimbali walijiunga na Israeli wakawa waongofu Wayahudi.
-