-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Lakini mabawa mawili ya tai akapewa mwanamke, ili yeye apate kuruka kwenda katika jangwa kwenye mahali pake; huko ndiko yeye analishwa kwa wakati na nyakati na nusu wakati mbali na uso wa nyoka.”—Ufunuo 12:13, 14, NW.
-
-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
24. Ni nini kilichopata Wanafunzi wa Biblia kilichofanana na kukombolewa kwa Waisraeli kutoka Misri?
24 Vita ya ulimwengu ya kwanza ilipokuwa ikipiganwa, ndugu waaminifu wa Yesu waliendelea na kushuhudu kwao kadiri walivyoweza. Hiyo ilifanywa usoni mwa upinzani ulioongezewa mkazo kutoka Shetani na vibaraka wake wakali. Mwishowe, kushuhudu peupe kwa Wanafunzi wa Biblia karibu kulisimamishwa. (Ufunuo 11:7-10) Hiyo ilikuwa wakati walipopatwa na kituko kama kile cha Waisraeli katika Misri ambao pia walivumilia chini ya uonevu mkubwa. Ikawa ndipo Yehova alipowaleta upesi, kama kwa mabawa ya tai, kwenye usalama katika jangwa la Sinai. (Kutoka 19:1-4) Hali kadhalika, baada ya mnyanyaso mkali wa 1918-19, Yehova alikomboa mashahidi wake, wenye kuwakilisha mwanamke wake, akawaingiza ndani ya hali ya kiroho iliyokuwa salama kwao kama jangwa lilivyokuwa kwa Waisraeli. Hiyo ilikuja ikiwa jibu la sala zao.—Linga Zaburi 55:6-9.
-