-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
25. (a) Ni nini alichotokeza Yehova katika 1919, kama alivyotokeza Waisraeli wakiwa taifa jangwani? (b) Ni nani wanaojumlika kuwa taifa hili, nao wameletwa ndani ya nini?
25 Huko jangwani, Yehova aliwatokeza Waisraeli wakiwa taifa, akiwaandalia kiroho na kimwili. Hali moja na hiyo, kuanzia 1919, Yehova aliitokeza mbegu ya mwanamke ikiwa taifa la kiroho. Hili lisifikiriwe kuwa ule Ufalme wa Kimesiya ambao umekuwa ukitawala kutoka katika mbingu tangu 1914. Badala ya hivyo, washiriki wa hili taifa jipya ni baki la mashahidi wapakwa-mafuta walio duniani, walioletwa ndani ya hali ya kiroho tukufu katika 1919. Wakiwa sasa wanaandaliwa “kipimo cha ugavi wa chakula chao kwa wakati unaofaa,” hao waliimarishwa kwa ajili ya kazi iliyokuwa mbele.—Luka 12:42, NW; Isaya 66:8.
26. (a) Kile kipindi cha wakati kinachotajwa kwenye Ufunuo 12:6, 14 ni cha urefu gani? (b) Ni nini lililokuwa kusudi la kipindi hicho cha nyakati tatu na nusu, kilianza lini na kilikwisha lini?
26 Pumziko la muda hili la mbegu ya mwanamke wa Mungu lilidumu kwa muda gani? Ufunuo 12:6 husema siku 1,260. Ufunuo 12:14 hukiita kipindi hicho wakati, nyakati, na nusu wakati; kwa maneno mengine, nyakati tatu na nusu. Kwa kweli, semi zote mbili husimamia miaka mitatu na nusu, ikiendelea katika Kizio cha Kaskazini kutoka masika ya 1919 kufika vuli ya 1922. Hiki kilikuwa kipindi cha ponyo lenye kuburudisha na kujipanga tena kitengenezo kwa jamii ya Yohana iliyorudishwa.
-
-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
1919-1922 Kipindi cha kupona
-