Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Yeremia
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Machi 15
    • Neno la Yehova Liko Hai

      Mambo Makuu Katika Kitabu cha Yeremia

      YEREMIA aliwatangazia watu wake mwenyewe misiba yenye kushtua kama nini! Hekalu tukufu ambalo lilikuwa kitovu cha ibada kwa zaidi ya karne tatu lingeteketezwa kabisa. Jiji la Yerusalemu na nchi ya Yuda zingeachwa ukiwa, na wakaaji wake kupelekwa uhamishoni. Masimulizi kuhusu matukio hayo na matangazo mengine ya hukumu yamo katika kitabu cha pili kwa ukubwa cha Biblia, yaani, kitabu cha Yeremia. Pia, kinasimulia mambo yaliyompata Yeremia alipokuwa akitimiza kwa uaminifu huduma yake iliyodumu kwa miaka 67. Habari zilizo katika kitabu hicho, hazijapangwa kulingana na tarehe ya matukio, bali kulingana na ujumbe wake.

  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Yeremia
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Machi 15
    • “MAMBO MAWILI MABAYA AMBAYO WATU WANGU WAMEFANYA”

      (Yeremia 1:1–20:18)

      Yeremia anawekwa kuwa nabii katika mwaka wa 13 wa utawala wa Yosia, mfalme wa Yuda, yaani, miaka 40 kabla ya uharibifu wa Yerusalemu mwaka wa 607 K.W.K. (Yeremia 1:1, 2) Matangazo yaliyotolewa hasa katika miaka 18 ya mwisho ya utawala wa Yosia yanaonyesha ubaya wa Yuda na kutangaza hukumu za Yehova juu ya Yuda. “Nami nitafanya Yerusalemu kuwa rundo la mawe,” Yehova anasema, “na majiji ya Yuda nitayafanya kuwa mahame yenye ukiwa, bila mkaaji.” (Yeremia 9:11) Kwa nini? “Kwa sababu kuna mambo mawili mabaya ambayo watu wangu wamefanya,” Yehova anasema.—Yeremia 2:13.

      Ujumbe huo unahusu pia kurudishwa kwa mabaki wenye kutubu. (Yeremia 3:14-18; 12:14, 15; 16:14-21) Hata hivyo, mjumbe huyo hapokelewi vizuri. “Msimamizi mkuu katika nyumba ya Yehova” anampiga Yeremia na kumtia katika mikatale usiku wote.—Yeremia 20:1-3.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki