-
Jihadhari na Moyo Wenye HilaMungu Asema Nasi Kupitia Yeremia
-
-
17-19. (a) Kwa nini Yeremia alifunga safari ndefu kwenda Efrati? (b) Utii wa Yeremia ulijaribiwa jinsi gani? (c) Yote ambayo Yeremia alifanya kuhusiana na mshipi yalitimiza nini?
17 Ili kuutimiza mgawo wake ifaavyo, Yeremia alipaswa kutii mwongozo wa Mungu. Kama ungekuwa Yeremia, je, ungefuata maagizo aliyopewa? Pindi moja, Yehova alimwambia Yeremia atafute mshipi wa kitani na ajifunge kiunoni. Kisha, Mungu akamwamuru asafiri mpaka Efrati. Ukitazama ramani, utaona kwamba alipaswa kusafiri kilomita 500 hivi. Baada ya kufika huko, Yeremia alipaswa kuuficha mshipi huo katika mpasuko wa mwamba kisha arudi Yerusalemu. Baadaye, Mungu alimwagiza afunge safari hiyo tena kwenda kuuchukua. (Soma Yeremia 13:1-9.) Kwa ujumla, huenda Yeremia alisafiri kilomita 1,900 hivi. Wachambuzi wa Biblia hudai haiwezekani kwamba alisafiri mbali hivyo, kwa miezi kadhaa.b (Ezra 7:9) Hata hivyo, hilo lilikuwa agizo la Mungu naye Yeremia alitii.
18 Wazia nabii huyo akipanda na kushuka milima ya Yudea, kisha akipitia jangwani kuelekea Efrati, ikitegemea njia aliyopitia. Kwa kusudi gani? Ili tu kwenda kuuficha mshipi wa kitani! Haikosi kutoweka kwake kwa muda mrefu kuliwashangaza jirani zake. Aliporudi, hakuwa na ule mshipi wa kitani. Kisha Mungu akamwambia afunge safari tena kwenda kuuchukua ule mshipi ambao sasa ulikuwa umeoza na “haufai jambo lolote.” Ingalikuwa rahisi kwake kusema: ‘Sasa imezidi. Sioni haja!’ Hata hivyo, kwa kuwa alikuwa amefinyangwa na Mungu, hakusema hivyo. Badala ya kulalamika, alifanya vile alivyoagizwa!
Kwa nini tunapaswa kutii maagizo ya Yehova hata ikiwa hatuyaelewi?
19 Baada ya kwenda na kurudi mara ya pili, ndipo Mungu alipofafanua mambo. Baada ya Yeremia kufanya yote hayo, sasa angeweza kutangaza ujumbe huu muhimu: “Watu hawa wabaya wanaokataa kuyatii maneno yangu, wanaotembea katika ukaidi wa moyo wao na wanaoendelea kufuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiinamia, pia watakuwa kama mshipi huu ambao haufai kwa jambo lolote.” (Yer. 13:10) Yehova alitumia njia bora kama nini ili kuwafundisha watu wake! Utii wa Yeremia wa kutoka moyoni katika jambo ambalo lilionekana kuwa dogo ulitimiza fungu muhimu katika jitihada za Yehova za kufikia mioyo ya watu wake.—Yer. 13:11.
-
-
Jihadhari na Moyo Wenye HilaMungu Asema Nasi Kupitia Yeremia
-
-
b Wengine hudai kwamba mahali ambapo Yeremia alienda palikuwa karibu wala si Efrati. Kwa nini? “Msingi pekee wa kudai hivyo,” asema msomi mmoja, “ni kumwepusha nabii huyo na safari mbili ndefu kutoka Yerusalemu mpaka Efrati.”
-