Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Utachagua Marafiki wa Aina Gani?
    Mungu Asema Nasi Kupitia Yeremia
    • 3. Sedekia alitaka nini kutoka kwa Yeremia, naye Yeremia alifanya nini?

      3 Mara kadha wa kadha, Mfalme Sedekia alitafuta ushauri wa Yeremia kabla ya Yerusalemu kuharibiwa. Kwa nini? Mfalme huyo alitazamia kupata majibu yenye kutia moyo kuhusu wakati ujao wa utawala wake. Alitaka Yeremia atangaze kwamba Mungu ataingilia kati na kukomboa Yuda kutoka kwa maadui wake. Kupitia wajumbe, Sedekia alimsihi Yeremia: “Tafadhali muulize Yehova kwa ajili yetu, kwa sababu Nebukadreza mfalme wa Babiloni anapiga vita juu yetu. Labda Yehova atatutendea kulingana na kazi zake zote za ajabu, hivi kwamba [Nebukadreza] aondoke kwetu.” (Yer. 21:2) Mfalme huyo hakutaka kufuata mwongozo wa Mungu wa kujitia mikononi mwa Babiloni. Msomi mmoja alimfananisha Sedekia na “mgonjwa anayerudi kwa daktari tena na tena ili kuhakikishiwa kwamba atapona, lakini hataki kutumia dawa alizoandikiwa.” Namna gani Yeremia? Angeweza kumfurahisha Sedekia kwa kumwambia alichotaka kusikia. Kwa nini basi Yeremia hakubadili ujumbe wake na kujirahisishia mambo? Alikataa kufanya hivyo kwa sababu Yehova alikuwa amemwambia atangaze kwamba jiji la Yerusalemu litaanguka.—Soma Yeremia 32:1-5.

      Picha katika ukurasa wa 54, 55

      Unaposoma kuhusu Yeremia na Ebed-meleki, je, unaamini kwamba walikuwa watu halisi? Hivi majuzi, masimulizi ya Yeremia sura ya 38 yanayowataja yaliungwa mkono na machimbuzi mawili yaliyofanywa katika Jiji la Daudi la kale.

      Mtaalamu wa vitu vya kale, Eilat Mazar anaripoti kwamba alichimbua kipande cha udongo chenye alama za muhuri. (chini kushoto) Kilipatikana mwaka wa 2005, uchimbuzi wa tabaka la wakati ambapo Yerusalemu liliharibiwa mwaka wa 607 K.W.K. Kipande hicho kina jina la kale la Kiebrania “Yehuchal ben Shelemyahu,” yaani, “Yukali mwana wa Shelemia” katika Kiswahili.

      Baadaye, katika tabaka lingine kama hilo, mita chache tu karibu na lile la kwanza, kipande kingine kilichimbuliwa. (chini kulia) Kipande hicho kina jina “Gedalyahu ben Pashhur,” au “Gedalia mwana wa Pashuri.”

      Sasa soma andiko la Yeremia 38:1 lenye majina ya wakuu wawili waliomsihi Mfalme Sedekia aagize Yeremia auawe, njama iliyozuiwa na Ebed-meleki. Ndiyo, wale wanaotajwa katika Yeremia sura ya 38 ni watu halisi.

  • Utachagua Marafiki wa Aina Gani?
    Mungu Asema Nasi Kupitia Yeremia
    • Yeremia hangeweza kukatiza kabisa ushirikiano wake na Sedekia; hata wakati ambapo Sedekia alikataa kufuata shauri la Mungu, bado ndiye aliyekuwa mfalme. Hata hivyo, haikumaanisha kwamba lazima Yeremia afuate maoni yaliyopotoka ya mfalme au kumpendeza. Ni kweli kwamba kama Yeremia angefanya jinsi mfalme alivyotaka, Sedekia angeweza kumpa zawadi nyingi na kumfaa kwa njia nyinginezo. Badala yake, Yeremia alikataa kushinikizwa kuwa rafiki ya Sedekia. Kwa nini? Kwa sababu Yeremia hakuwa tayari kulegeza msimamo ambao Yehova alikuwa amemwambia achukue.

      Picha katika ukurasa wa 57
Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki