Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Unapaswa Kuwa Wapi Mwisho Unapokuja?
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Mei 15
    • Pia, fikiria kisa cha Rahabu, kahaba aliyeishi katika jiji la Yeriko. Waisraeli walikuwa karibu kuanza vita vya kuimiliki Nchi ya Ahadi. Rahabu alipotambua kwamba jiji la Yeriko lingeharibiwa, aliwaambia wapelelezi wawili Waisraeli kwamba wakaaji wa jiji walikuwa wamevunjika moyo kwa kuwa waliogopa Waisraeli waliokuwa wakikaribia sana. Aliwaficha wapelelezi hao na kuwaomba wamwapie kuwa wangemlinda hai yeye na familia yake yote wakati ambapo jiji la Yeriko lingeharibiwa. Wapelelezi hao walimwagiza Rahabu akusanye pamoja watu wa familia yake ndani ya nyumba yake, iliyokuwa imejengwa kwenye ukuta wa jiji. Ikiwa wangetoka nje ya nyumba wangeharibiwa pamoja na watu wengine wa jiji hilo. (Yos. 2:8-13, 15, 18, 19) Hata hivyo, baadaye Yehova alimwambia Yoshua hivi: “Ukuta wa jiji utaanguka chini.” (Yos. 6:5) Sasa mahali ambapo wapelelezi walisema kuwa pangekuwa salama palionekana kuwa hatari. Rahabu na watu wa familia yake wangeokolewa jinsi gani?

      Wakati ulipofika wa kuteka Yeriko, Waisraeli walipiga kelele nao wakaanza kupuliza pembe. Andiko la Yoshua 6:20 linasema hivi: “Ikawa kwamba mara tu watu [wa Israeli] walipoisikia sauti ya pembe na watu wakapaaza kelele kubwa za vita, ndipo ukuta ukaanza kuanguka chini kabisa.” Hakuna mwanadamu yeyote angeweza kuuzuia ukuta huo usianguke. Hata hivyo, kwa muujiza, ukuta wa jiji hilo haukuendelea kuanguka ulipofika kwenye nyumba ya Rahabu. Yoshua akawaamuru wale wapelelezi wawili: “Ingieni katika nyumba ya yule mwanamke, yule kahaba, mkamtoe nje mwanamke huyo na wote walio wake, kama vile mlivyomwapia.” (Yos. 6:22) Watu wote waliokuwa ndani ya nyumba ya Rahabu waliokolewa.

  • Unapaswa Kuwa Wapi Mwisho Unapokuja?
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Mei 15
    • Kuokoka kwa Waisraeli huko Misri na Rahabu katika jiji la Yeriko, kulitegemea kubaki ndani ya nyumba zao. Hilo lilihitaji imani na utii. (Ebr. 11:28, 30, 31) Fikiria jinsi kila familia ya Waisraeli ilivyoendelea kumkazia macho mzaliwa wao wa kwanza ‘kilio kikubwa kilipoanza kutokea’ katika nyumba moja baada ya nyingine ya Wamisri. (Kut. 12:30) Fikiria jinsi Rahabu alivyojikunyata pamoja na familia yake aliposikia mngurumo wa kuta za Yeriko zilizokuwa zikianguka ukikaribia nyumba yake zaidi na zaidi. Alihitaji kuwa na imani sana ili kubaki mtiifu na kukaa ndani ya nyumba hiyo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki