Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Hatawaacha Washikamanifu Wake
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Agosti 15
    • Yehova Hatawaacha Washikamanifu Wake

      “[Yehova] hatawaacha washikamanifu wake. Hakika watalindwa mpaka wakati usio na kipimo.”—ZAB. 37:28.

      1, 2. (a) Ni mambo gani yaliyojaribu ushikamanifu wa watumishi wa Mungu katika karne ya kumi K.W.K.? (b) Yehova aliwalinda washikamanifu wake katika hali gani tatu?

      NI KARNE ya kumi K.W.K. na ni wakati wa kufanya uamuzi. Vita vya wenyewe kwa wenyewe vimeepukwa chupuchupu wakati makabila ya kaskazini ya Israeli yenye msukosuko yanapopewa uhuru wa kadiri fulani. Yeroboamu, mfalme wao aliyewekwa rasmi hivi karibuni tu, anaimarisha haraka mamlaka yake kwa kuanzisha dini mpya ya taifa. Anataka raia wake wamtii kikamili. Watumishi waaminifu wa Yehova watafanya nini? Je, watabaki washikamanifu kwa Mungu wanayemwabudu? Maelfu wanafanya hivyo, na Yehova anawalinda wanapodumisha utimilifu wao.—1 Fal. 12:1-33; 2 Nya. 11:13, 14.

  • Yehova Hatawaacha Washikamanifu Wake
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Agosti 15
    • 5, 6. Kulikuwa na matokeo gani Sulemani alipoacha kuwa mshikamanifu kwa Mungu?

      5 Alipozeeka, Sulemani aliacha kuwa mwaminifu kwa Yehova naye akaanza kushiriki katika ibada ya uwongo. (1 Fal. 11:4-6) Hatua kwa hatua, Sulemani aliacha kutii sheria za Yehova na akawakandamiza sana watu. Aliwakandamiza watu sana hivi kwamba baada ya kifo chake, watu waliendelea kulalamika kumhusu kwa mwana na mrithi wake, Rehoboamu, na kumwomba awapunguzie nira nzito. (1 Fal. 12:4) Yehova alihisi jinsi gani Sulemani alipoacha kuwa mwaminifu?

      6 Biblia inatuambia hivi: “Yehova akamkasirikia Sulemani, kwa sababu moyo wake ulikuwa umegeuka ukamwacha . . . Mungu wa Israeli, yeye aliyemtokea mara mbili.” Yehova akamwambia Sulemani: “Kwa sababu . . . hukushika agano langu na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme kutoka kwako, nami nitampa mtumishi wako.”—1 Fal. 11:9-11.

      7. Ingawa Sulemani alikataliwa, Yehova aliwajali jinsi gani washikamanifu Wake?

      7 Kisha, Yehova akamtuma nabii Ahiya amtie mafuta mkombozi. Mkombozi huyo alikuwa Yeroboamu, mwanamume mwenye uwezo aliyefanya kazi katika serikali ya Sulemani. Ingawa Yehova alibaki mshikamanifu kwa agano la Ufalme alilofanya na Daudi, Alikubali serikali ya makabila 12 igawanyike. Yeroboamu angepewa makabila kumi; na mawili yangebaki katika familia ya ukoo wa Daudi, ambayo sasa iliwakilishwa na Mfalme Rehoboamu. (1 Fal. 11:29-37; 12:16, 17, 21) Yehova alimwambia Yeroboamu hivi: “Itatukia kwamba, ukitii yote ambayo nitakuamuru, nawe utembee katika njia zangu na kwa kweli ufanye yaliyo sawa machoni pangu kwa kushika sheria zangu na amri zangu, kama Daudi mtumishi wangu alivyofanya, mimi pia nitakuwa pamoja nawe, nami nitakujengea nyumba yenye kudumu, kama nilivyomjengea Daudi, nami nitakupa Israeli.” (1 Fal. 11:38) Yehova alichukua hatua ili kuwasaidia watu wake naye akatayarisha njia ili kuwatoa katika ukandamizaji huo.

  • Yehova Hatawaacha Washikamanifu Wake
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Agosti 15
    • 11. Yeroboamu aliacha jinsi gani kuwa mshikamanifu?

      11 Utawala wa Mfalme Yeroboamu ungewaletea watu wa Mungu kitulizo fulani. Badala yake, matendo yake yalijaribu hata zaidi ushikamanifu wao kwa Mungu. Kwa kuwa hakuridhika na heshima na pendeleo alilokuwa tayari amepewa, Yeroboamu alianza kutafuta njia za kuimarisha cheo chake. Alifikiri hivi: “Watu hawa wakiendelea kwenda kutoa dhabihu katika nyumba ya Yehova huko Yerusalemu, moyo wa watu hawa pia utarudi kwa bwana wao, Rehoboamu mfalme wa Yuda; nao hakika wataniua na kurudi kwa Rehoboamu mfalme wa Yuda.” Hivyo, Yeroboamu akaanzisha dini mpya iliyotegemea ndama wawili wa dhahabu. “Kisha akaweka mmoja kule Betheli, na mwingine akamweka kule Dani. Na jambo hilo likaja kusababisha dhambi, na watu wakaanza kwenda mpaka kule Dani mbele ya yule aliyekuwa huko. Naye akaanza kujenga nyumba ya mahali pa juu na kuweka makuhani kutoka kwa watu wa kawaida, ambao hawakuwa wa wana wa Lawi.” Yeroboamu hata akaanzisha siku yake mwenyewe ya “sherehe kwa ajili ya wana wa Israeli,” naye akaanza “kutoa matoleo juu ya madhabahu ili kufukiza moshi wa dhabihu.”—1 Fal. 12:26-33.

      12. Washikamanifu wa Mungu katika ufalme wa kaskazini walifanya nini Yeroboamu alipoanzisha ibada ya ndama huko Israeli?

      12 Sasa washikamanifu wa Mungu katika ufalme wa kaskazini wangefanya nini? Walawi waliokuwa wakiishi katika majiji waliyopewa katika eneo la ufalme wa kaskazini walichukua hatua mara moja kama walivyofanya mababu wao waaminifu. (Kut. 32:26-28; Hes. 35:6-8; Kum. 33:8, 9) Waliacha urithi wao wote, wakahamishia familia zao kusini huko Yuda, ambako wangeendelea kumwabudu Yehova bila vipingamizi. (2 Nya. 11:13, 14) Waisraeli wengine ambao walikuwa wakiishi kwa muda huko Yuda waliamua kubaki Yuda badala ya kurudi nyumbani. (2 Nya. 10:17) Yehova alihakikisha kwamba njia ya kurudia ibada ya kweli iliachwa wazi ili katika vizazi vya baadaye wengine kutoka katika ufalme wa kaskazini waweze kuacha ibada ya ndama na kurudi Yuda.—2 Nya. 15:9-15.

  • Yehova Hatawaacha Washikamanifu Wake
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Agosti 15
    • 16. Nabii fulani kutoka Yuda alipewa mgawo gani?

      16 Yehova alimhukumu Yeroboamu kwa sababu ya uasi-imani. Yehova alimtuma nabii fulani kutoka Yuda aende kaskazini mpaka Betheli ili amwone Yeroboamu alipokuwa akifukiza moshi wa dhabihu kwenye madhabahu. Nabii huyo alipaswa kumpa Yeroboamu ujumbe wa hukumu wenye kushtua. Bila shaka, huo ulikuwa mgawo mgumu.—1 Fal. 13:1-3.

      17. Yehova alimlinda mjumbe wake jinsi gani?

      17 Yeroboamu alikasirika sana aliposikia hukumu ya Yehova. Akamnyooshea mkono mwakilishi wa Mungu na kuwapaazia sauti wanaume waliokuwa karibu, akisema: “Mkamateni!” Lakini papo hapo, kabla mtu yeyote hajatenda, ‘mkono aliomnyooshea ukapooza, naye hakuweza kuurudisha nyuma kwake. Na ile madhabahu ikapasuka hivi kwamba majivu yenye mafuta yakamwagika kutoka katika madhabahu.’ Yeroboamu alilazimika kumwomba nabii huyo autulize uso wa Yehova na kusali ili mkono huo uliopooza uponywe. Nabii huyo alifanya hivyo, na mkono ukapona. Hivyo, Yehova alimlinda mjumbe wake asipatwe na madhara.—1 Fal. 13:4-6.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki