Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yule Mwanamke Tasa Ashangilia
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 2. Kwa nini unabii ulioandikwa katika Isaya sura ya 54 utupendeze?

      2 Shida ya Sara hutusaidia kuuelewa unabii ulioandikwa katika Isaya sura ya 54. Humo Yerusalemu anaambiwa mambo kana kwamba ni mwanamke tasa anayepata shangwe kubwa ya kuwa na watoto wengi. Yehova anawaonyesha watu wake wa kale hisia nyororo kwa kuwataja wote kwa ujumla kuwa mke wake wa mfano.

  • Yule Mwanamke Tasa Ashangilia
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 3. Kwa nini “mwanamke” huyo tasa atakuwa na sababu ya kushangilia?

      3 Sura ya 54 inaanza kwa hali ya furaha: “Imba, wewe [“mwanamke,” “NW”] uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto [“wana,” “NW”] wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA.” (Isaya 54:1) Isaya anasisimuka kama nini kusema maneno hayo! Na utimizo wake utawaletea faraja iliyoje Wayahudi walioko uhamishoni Babiloni! Wakati huo Yerusalemu bado atakuwa ukiwa. Kwa maoni ya kibinadamu, itaonekana ni kama hakuna kamwe tumaini la jiji hilo kukaliwa na watu tena, sawa na vile isivyo kawaida mwanamke tasa kutumainia kuzaa watoto siku za uzeeni. Lakini “mwanamke” huyu ana baraka kubwa wakati wake ujao—atapata nguvu za uzazi. Yerusalemu atachachawa kwa shangwe ya ajabu. Atamiminikwa tena na “wana,” au wakaaji.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki