Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kumtambua Mjumbe wa Aina Inayofaa
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Mei 1
    • 2. Ni hitilafiano gani kati ya wajumbe lililotukia katika nyakati za Israeli?

      2 Wote wawili Isaya na Ezekieli walidai kuwa wajumbe wa Yehova Mungu. Je, ndivyo ilivyokuwa? Acheni tuone. Isaya alitabiri katika Yerusalemu tangu 778 K.W.K. hivi hadi wakati fulani baada ya 732 K.W.K. Ezekieli alikuwa mateka katika Babiloni mwaka wa 617 K.W.K. Aliwatabiria ndugu zake Wayahudi huko. Manabii wote wawili walitangaza kwa ujasiri kwamba Yerusalemu lingeharibiwa. Manabii wengine walisema kwamba Mungu hangeruhusu hilo litukie. Ni nani waliothibitika kuwa wajumbe wa aina inayofaa?

  • Kumtambua Mjumbe wa Aina Inayofaa
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Mei 1
    • 5, 6. Wajapokuwa wajumbe wote wasio wa kweli, Isaya alitetewaje kuwa nabii wa kweli?

      5 Kwa habari ya Isaya, ujumbe wake wote mbalimbali wa kimungu juu ya Yerusalemu ulitimia. Kwenye kiangazi cha 607 K.W.K., Wababiloni waliharibu hilo jiji, wakarudi Babiloni na baki la Kiyahudi likiwa mateka. (2 Mambo ya Nyakati 36:15-21; Ezekieli 22:28; Danieli 9:2) Je, misiba hiyo iliwazuia manabii wasio wa kweli wasishambulie watu wa Mungu wakiwa na usemi wa ubatili? La, wajumbe hao wenye kusema uwongo waliendelea kufanya hivyo!

      6 Kana kwamba hilo halikutosha, Waisraeli waliokuwa mateka walipatwa pia na maoni ya watabiri wenye kujivuna, waaguzi, na wanajimu wa Babiloni. Hata hivyo, Yehova aliwathibitisha wajumbe wote hao wasio wa kweli kuwa wapumbavu walioshindwa, wenye kutoa unabii kinyume cha kile ambacho kingetukia. Kwa wakati ufaao yeye alionyesha kwamba Ezekieli alikuwa mjumbe wake wa kweli, kama alivyokuwa Isaya. Yehova alitimiza maneno yote aliyosema kupitia wao, kama tu alivyokuwa ameahidi: “Nazibatilisha ishara za waongeao upuzi, nami ndiye Yule ambaye hufanya waaguzi wenyewe watende kwa kichaa; Yule ageuzaye watu wenye hekima nyuma, na Yule ambaye hugeuza hata ujuzi wao kuwa upumbavu; Yule afanyaye neno la mtumishi wake litimie, na Yule ambaye hutekeleza kikamili shauri la wajumbe wake mwenyewe.”—Isaya 44:25, 26, NW.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki