Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Imani Katika Unabii wa Biblia Inaokoa Uhai
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Aprili 1
    • Wakati Maliki Nero wa Roma anapokufa, Vespasian anaenda Roma kuchukua kiti cha ufalme, anamwacha Tito amalize kampeni ya kushambulia Yudea. Tito anashambulia Yerusalemu karibu Pasaka ya mwaka wa 70 W.K., akiwanasa jijini humo wakaaji na wasafiri waliotoka maeneo mengine. Majeshi yake yanakata miti katika maeneo ya mashambani ya Yudea ili kujenga ukuta wenye miti iliyochongoka. Wanajenga ukuta huo umbali wa kilomita 7 kuzunguka jiji hilo. Ni kama tu Yesu alivyotabiri: ‘Adui zako watajenga kukuzunguka ngome yenye miti iliyochongoka nao watakuzunguka na kukutaabisha kutoka kila upande.’—Luka 19:43.

      Punde si punde, kunakuwa na njaa kali jijini. Vikundi vyenye silaha vinapora nyumba za watu waliouawa na za wale wanaokufa. Angalau mwanamke mmoja mwenye njaa kali anamuua na kumla mtoto wake mchanga, na hivyo anatimiza unabii uliosema: “Utalazimika kula uzao wa tumbo lako, nyama ya wana wako na binti zako . . . kwa sababu ya mbano na mkazo ambao adui yako atakusonga nao.”—Kumbukumbu la Torati 28:53-57.

      Mwishowe, baada ya kuzingirwa kwa miezi mitano, Yerusalemu linaanguka. Jiji hilo na hekalu lake kubwa linaporwa na kuteketezwa kisha, linabomolewa jiwe kwa jiwe. (Danieli 9:26) Jumla ya watu 1,100,000 hivi wanakufa; na wengine 97,000 wanauzwa utumwani.b (Kumbukumbu la Torati 28:68) Yudea linabaki karibu ukiwa bila Wayahudi. Kwa kweli, huo ni msiba wa kitaifa ambao hauna kifani. Maisha ya kisiasa, kidini, na ya kitamaduni ya Wayahudi yanabadilika kabisa.c

  • Imani Katika Unabii wa Biblia Inaokoa Uhai
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Aprili 1
    • b Kulingana na kadirio moja, zaidi ya Myahudi mmoja kwa kila Wayahudi 7 aliuawa katika Milki ya Roma.

      c Alfred Edersheim, msomi wa Biblia Myahudi aliandika hivi: “Dhiki [hiyo] iliyokumba Israeli [haikuwa] na kifani katika historia yake ya matukio mabaya sana, na haingelinganishwa kamwe na misiba iliyotukia baadaye.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki