-
Je, Kweli Mungu Anawajali Wanawake?Mnara wa Mlinzi—2012 | Septemba 1
-
-
Maoni ya Mungu Kuhusu Wanawake Yapotoshwa
Chini ya Sheria ya Musa, wanawake walitendewa kwa heshima na haki zao ziliheshimiwa. Hata hivyo, kuanzia karne ya nne K.W.K., dini ya Kiyahudi ilianza kuiga tamaduni za Wagiriki, ambao waliwaona wanawake kuwa duni.—Ona sanduku lenye kichwa “Ubaguzi Dhidi ya Wanawake Katika Maandishi ya Kale.”
Kwa mfano, mtunga-mashairi Mgiriki Hesiod (aliyeishi karne ya nane K.W.K.) aliwalaumu wanawake kwa sababu ya matatizo yote yanayowapata wanadamu. Katika shairi lake linaloitwa Theogony, alizungumza kuhusu “jamii na kabila hatari la wanawake ambao wanaishi katikati ya wanaume na kuwasababishia matatizo mengi.” Wazo hilo liliingizwa katika dini ya Kiyahudi mwanzoni mwa karne ya pili K.W.K. Talmud, ambayo ilianza kuandikwa katika karne ya pili W.K. na kuendelea, iliwaonya wanaume hivi: “Msizungumze sana na wanawake, kwa sababu hilo litawaingiza katika upotovu wa maadili.”
Kwa karne nyingi, maoni hayo yaliyopotoka yameathiri sana daraka la wanawake katika jamii ya Wayahudi. Katika siku za Yesu, tayari wanawake walikuwa wamewekewa mipaka kwenye eneo la hekalu na waliruhusiwa tu kuingia kwenye Ua wa Wanawake. Wanaume tu ndio waliopokea elimu ya kidini, na inaelekea wanawake walitengwa na wanaume kwenye masinagogi. Talmud inanukuu maneno haya ya Rabi mmoja: “Yeyote anayemfundisha binti yake Torati [Sheria] anamfundisha mambo machafu.” Kwa kupotosha maoni ya Mungu, viongozi wa kidini Wayahudi waliwafanya wanaume wengi wawadharau wanawake.
-