Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wahasmonia na Hali Waliyoacha
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Juni 15
    • Mafarisayo na Masadukayo wanatokea kama watu wenye ushawishi mkubwa, wenye uwezo wa kubadili maoni ya watu hata kufikia hatua ya kumkataa Yesu kuwa Mesiya. (Mathayo 15:1, 2; 16:1; Yohana 11:47, 48; 12:42, 43) Hata hivyo, makundi hayo mawili yenye ushawishi hayatajwi popote katika Maandiko ya Kiebrania.

      Josephus anawataja Masadukayo na Mafarisayo mara ya kwanza katika karne ya pili K.W.K.

  • Wahasmonia na Hali Waliyoacha
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Juni 15
    • Mafarisayo na Masadukayo Watokea

      Anapoandika juu ya utawala wa Hyrcanus, ndipo Josephus kwanza anaandika juu ya uvutano unaozidi wa Mafarisayo na Masadukayo. (Josephus alikuwa ametaja Mafarisayo walioishi wakati wa utawala wa Jonathan.) Yeye hataji kama walikuwa na chanzo kimoja. Wasomi wengi wanaonelea kwamba walikuwa kikundi kilichotokana na Wasidim, madhehebu yenye kujitoa kwa Mungu iliyomwunga mkono Judah Maccabee katika kutimiza malengo yake ya kidini lakini wakamwacha wakati alipoanza kutamani mambo ya kisiasa.

      Kwa kawaida jina Mafarisayo linahusianishwa na neno la Kiebrania linalomaanisha “waliojitenga,” japo wengine huona kuwa linahusiana na neno “wafasiri.” Mafarisayo walikuwa wasomi walioishi miongoni mwa watu wa kawaida wasiokuwa na ukoo maalum. Walijitenga wasichafuliwe kidini, hivyo wakafuata falsafa ya utakatifu wa pekee na kutumia sheria za hekalu, ambazo zinahusiana na utakatifu wa kikuhani, katika hali za kawaida za maisha yao ya kila siku. Mafarisayo walitokeza njia mpya ya kufasiri Maandiko na dhana ambayo baadaye iliitwa sheria ya mdomo. Wakati wa utawala wa Simon walipata kuwa na uvutano mkubwa zaidi wakati baadhi yao walipoteuliwa kuwa washiriki wa Gerousia (baraza la wanaume wazee), ambalo baadaye liliitwa Sanhedrini.

      Josephus asimulia kwamba mwanzoni John Hyrcanus alikuwa mwanafunzi wa Mafarisayo na aliwaunga mkono. Hata hivyo, baadaye Mafarisayo walimkemea kwa kutoacha ukuhani wa cheo cha juu, jambo lililofanya afarakane nao kabisa. Hyrcanus alipiga marufuku sheria za kidini za Mafarisayo. Ili kuwaadhibu zaidi Mafarisayo, aliwaunga mkono Masadukayo waliokuwa wapinzani wao wa kidini.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki