-
Usahihi wa Biblia Unathibitishwa na Maktaba ya Kale ya UrusiMnara wa Mlinzi—2005 | Julai 15
-
-
Hati Muhimu za Biblia Kutoka Krimea
Kuna msomi mwingine aliyekuwa akitafuta hati za kale za Biblia ambaye alitajwa mapema. Yeye alikuwa nani? Miaka michache kabla Tischendorf hajarudi Urusi, Maktaba ya Milki ilipewa nafasi ya kununua hati nyingi sana, jambo lililompendeza sana maliki na kuwavutia wasomi kutoka sehemu zote za Urusi na Ulaya. Jambo hilo liliwashangaza sana. Waliletewa hati nyingi na vitabu vingine. Maandishi hayo yalikuwa na sehemu mbalimbali 2,412, kutia ndani hati na vitabu vya kukunjwa 975. Kati ya hizo kulikuwa na hati 45 za Biblia zilizoandikwa kabla ya miaka ya 900. Inastaajabisha kwamba hati zote hizo zilikuwa zimekusanywa na mtu mmoja tu aliyeitwa Abraham Firkovich, msomi Mkaraite ambaye wakati huo alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 70! Lakini Wakaraite walikuwa nani?b
Hilo lilikuwa jambo muhimu sana kwa Maliki. Urusi ilikuwa imetwaa maeneo yaliyokuwa yakitawaliwa na nchi nyingine. Hivyo, watu wa asili mbalimbali waliishi katika eneo la milki hiyo. Eneo maridadi la Krimea, kwenye pwani ya Bahari Nyeusi, lilikaliwa na watu waliodhaniwa kuwa Wayahudi lakini ambao walikuwa na mila za Waturuki na lugha yao ilifanana na Kitatari. Wakaraite hao walisema kwamba walikuwa wazao wa Wayahudi waliopelekwa uhamishoni huko Babiloni baada ya uharibifu wa Yerusalemu mwaka wa 607 K.W.K. Hata hivyo, tofauti na Wayahudi waliokuwa wafuasi wa dini ya Kiyahudi, walikataa Talmud na kukazia kusoma Maandiko. Wakaraite walioishi Krimea walitaka sana kumwonyesha maliki kwamba wao ni tofauti na Wayahudi waliokuwa wafuasi wa dini ya Kiyahudi, na hivyo walitarajia kupata kibali cha kipekee. Wakaraite walifikiri kwamba kwa kumpa Maliki hati za kale walizokuwa nazo wangemthibitishia kwamba walikuwa wazao wa Wayahudi waliokuwa wamehamia Krimea baada ya kutoka uhamishoni huko Babiloni.
Firkovich alianza kutafuta maandishi na hati za kale katika nyumba zilizojengwa kwa mawe yaliyochongwa katika miamba huko Chufut-Kale, Krimea. Wakaraite walikuwa wameishi na kuabudu katika nyumba hizo ndogo kwa miaka mingi. Wakaraite hawakuharibu kamwe nakala zilizochakaa za Maandiko zilizokuwa na jina la Mungu, Yehova, kwa sababu waliona hilo kuwa tendo la kufuru. Hati zilizochakaa zilihifadhiwa katika ghala ndogo kwenye sinagogi lililoitwa geniza, ambalo ni neno la Kiebrania linalomaanisha “maficho.” Wakaraite hawakuziharibu hati hizo kamwe kwa sababu waliliheshimu sana jina la Mungu.
Ingawa hati hizo zilifunikwa kwa mavumbi kwa karne nyingi, Firkovich aliyachunguza maghala hayo kwa makini. Katika ghala moja alipata hati maarufu ya mwaka wa 916 W.K. Hati hiyo inaitwa Kodeksi ya Petersburg ya Manabii wa Mwisho nayo ni mojawapo ya nakala za kale zaidi za Maandiko ya Kiebrania.
Firkovich alikusanya hati nyingi sana na mwaka wa 1859 akaamua kuiuzia Maktaba ya Milki hati hizo. Mwaka wa 1862, Aleksanda wa Pili alisaidia kununua hati hizo kwa ajili ya maktaba hiyo kwa gharama kubwa sana, yaani rubo 125,000. Wakati huo gharama ya kuendesha maktaba hiyo haikuzidi rubo 10,000 kwa mwaka! Kodeksi ya Leningrad (B 19A) inayojulikana sana ilikuwa kati ya hati hizo zilizonunuliwa. Hati hiyo iliyoandikwa mwaka wa 1008 hivi ni nakala ya kale zaidi ya Maandiko yote ya Kiebrania. Msomi mmoja alisema kwamba “huenda hiyo ndiyo hati ya Biblia iliyo muhimu kuliko hati nyingine zote kwa sababu chapa nyingi za kisasa za Biblia ya Kiebrania zenye nyongeza zinategemea hati hiyo.”
-
-
Usahihi wa Biblia Unathibitishwa na Maktaba ya Kale ya UrusiMnara wa Mlinzi—2005 | Julai 15
-
-
[Picha katika ukurasa wa 12]
Abraham Firkovich
-