-
Mkono wa Yehova Haujawa MfupiUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
6. Matendo ya Jumuiya ya Wakristo yanafananaje na yale ya Yuda?
6 Ukosefu wa uadilifu na fujo zilizokuwa katika Yuda zina ulinganifu wa ajabu na zile zilizo katika Jumuiya ya Wakristo. (Ona “Jiji la Yerusalemu Lenye Uasi-Imani Linalingana na Jumuiya ya Wakristo,” katika ukurasa wa 294.) Vita viwili vikali vya ulimwengu vimepiganwa baina ya mataifa ambayo husemwa eti ni ya Kikristo. Hata sasa, ibada ya Jumuiya ya Wakristo imeshindwa kukomesha mauaji ya kufagilia mbali makabila fulani, na kuchinjana miongoni mwa washirika wake. (2 Timotheo 3:5) Ingawa Yesu aliwafundisha wafuasi wake kuutumaini Ufalme wa Mungu, mataifa ya Jumuiya ya Wakristo yanaendelea kutegemea silaha nyingi za kijeshi zilizojazana akibani, na kufanya mapatano ya kisiasa. (Mathayo 6:10) Kwa kweli, wengi wa watengenezaji wakuu wa silaha ulimwenguni wanapatikana katika mataifa ya Jumuiya ya Wakristo! Naam, hata Jumuiya ya Wakristo inatumainia “ubatili” kwa kutumainia jitihada za wanadamu na mashirika ili kupata usalama wa wakati ujao.
-
-
Mkono wa Yehova Haujawa MfupiUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
9. Kwa nini amani ya kweli imewaponyoka kabisa viongozi wa Jumuiya ya Wakristo?
9 Maneno haya yaliyopuliziwa yanatukumbusha jinsi ambavyo Jumuiya ya Wakristo imemwaga damu. Hakika, Yehova atamtoza hesabu kwa kuwakilisha Ukristo vibaya sana! Jumuiya ya Wakristo imefuatia mwendo ulio mpotovu kama wa Wayahudi wa siku za Isaya kwa sababu viongozi wake wanaamini kwamba huo tu ndio mwendo unaofaa. Huku wanasema amani, na huku wanatenda matendo yasiyo ya haki. Jamani, unafiki gani huo! Amani ya kweli itazidi tu kuwaponyoka kabisa viongozi wa Jumuiya ya Wakristo, maadamu wanaendelea kutumia mbinu hiyo. Ni kama vile unabii unavyoendelea kusema: “Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika miendo yao; wamejifanyizia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani.”—Isaya 59:8.
-