-
Jitihada za Kupinga Jina la MunguAmkeni!—2004 | Januari 22
-
-
Kitabu Encyclopaedia Judaica kinasema kwamba “watu waliepuka kutamka jina YHWH . . . kwa sababu ya kutoelewa Amri ya Tatu.” Amri ya tatu kati ya zile Amri Kumi ambazo Waisraeli walipewa na Mungu inasema: “Usilitumie jina la Yehova Mungu wako kwa njia isiyofaa, kwa maana Yehova hatamwacha bila kuadhibiwa yule anayelitumia jina lake kwa njia isiyofaa.” (Kutoka 20:7) Hivyo, amri ya Mungu iliyokataza jina la Mungu lisitumiwe kwa njia isiyofaa, ilipotoshwa na ikawa ushirikina.
Ama kwa hakika, hakuna yeyote leo anayedai kwamba Mungu angependa watu wachomwe kwa sababu ya kutamka jina Lake! Hata hivyo, watu wangali wanafuata maoni ya Wayahudi ya ushirikina kuhusu jina la Mungu. Wengi bado wanasema kwamba Tetragramatoni ni “Jina Lisilotamkika.” Watu wengine hutamka vibaya majina yote yanayomwakilisha Mungu kimakusudi ili wasivunje desturi hiyo. Kwa mfano Yah, ufupisho wa jina la Mungu, hutamkwa Kah. Haleluya hutamkwa Haleluka. Hata wengine huepuka kuandika jina “Mungu,” na badala yake hutumia kistari kuwakilisha herufi moja au zaidi. Kwa mfano, wanapotaka kuandika neno la Kiswahili “Mungu,” wao huandika “M-ngu.”
-
-
Jitihada za Kupinga Jina la MunguAmkeni!—2004 | Januari 22
-
-
kwa sababu ya desturi za wanadamu bali si mafundisho ya Biblia. Mtafiti Myahudi Tracey R. Rich, mwandishi wa kituo cha Judaism 101 cha Internet, anasema: “Hakuna chochote katika Torah kinachomkataza mtu kutamka Jina la Mungu. Maandiko yanaonyesha wazi kwamba Jina la Mungu lilitamkwa mara nyingi.”
-