Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Kweli Mungu Anawajali Wanawake?
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Septemba 1
    • Hata hivyo, kuanzia karne ya nne K.W.K., dini ya Kiyahudi ilianza kuiga tamaduni za Wagiriki, ambao waliwaona wanawake kuwa duni.​—Ona sanduku lenye kichwa “Ubaguzi Dhidi ya Wanawake Katika Maandishi ya Kale.”

      Kwa mfano, mtunga-mashairi Mgiriki Hesiod (aliyeishi karne ya nane K.W.K.) aliwalaumu wanawake kwa sababu ya matatizo yote yanayowapata wanadamu. Katika shairi lake linaloitwa Theogony, alizungumza kuhusu “jamii na kabila hatari la wanawake ambao wanaishi katikati ya wanaume na kuwasababishia matatizo mengi.” Wazo hilo liliingizwa katika dini ya Kiyahudi mwanzoni mwa karne ya pili K.W.K. Talmud, ambayo ilianza kuandikwa katika karne ya pili W.K. na kuendelea, iliwaonya wanaume hivi: “Msizungumze sana na wanawake, kwa sababu hilo litawaingiza katika upotovu wa maadili.”

  • Je, Kweli Mungu Anawajali Wanawake?
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Septemba 1
    • Kuanzia karne ya kwanza W.K. na kuendelea, waandikaji kama vile Filo wa Aleksandria walianza kutumia falsafa za Kigiriki ili kufafanua upya masimulizi ya kitabu cha Mwanzo. Filo alieleza kwamba Hawa alikuwa na dhambi ya kufanya ngono na kwa hiyo alihukumiwa kuwa na maisha ambayo “yangemnyima kabisa uhuru na kumweka chini ya ukandamizaji wa mwanamume.” Mtazamo kama huo wa kuwadharau wanawake uliingia katika dini ya Kiyahudi, na vilevile katika maandishi ya Mababa wa Kanisa.

      Katika maandishi ya Kiyahudi ya karne ya pili yanayoitwa Midrash Rabba, rabi fulani alieleza kwa nini alihisi kwamba wanawake wanapaswa kuvaa ushungi, alisema: “Mwanamke ni kama mtu ambaye amefanya makosa na anaaibika anapoona watu.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki