-
Je, Utatu Ni Fundisho la Biblia?Mnara wa Mlinzi—2012 | Machi 1
-
-
Andiko la Kumbukumbu la Torati 6:4 linataja hivi waziwazi: “Sikiliza, Ee Israeli: Yehova Mungu wetu ni Yehova mmoja”—si watatu katika mmoja. Taifa la Israeli lilikuwa limetoka tu kukombolewa kutoka Misri ambako miungu Osirisi, Isisi, na Horusi (inayoonyeshwa kushoto) iliabudiwa ikiwa mojawapo ya vikundi kadhaa vya miungu mitatu-mitatu. Hivyo, taifa la Israeli lilipewa amri ya kuabudu Mungu mmoja tu. Je, ilikuwa muhimu kwa watu kuelewa amri hiyo? Kulingana na Dakt. J. H. Hertz, ambaye ni rabi: “Tamko hilo lililo wazi la kuabudu Mungu mmoja tu lilikuwa tangazo la vita dhidi ya kuabudu miungu mingi . . . Katika njia hiyohiyo, Shema haitii ndani fundisho la utatu la imani ya Kikristo kwa kuwa linapinga Umoja wa Mungu.”a
-
-
Je, Utatu Ni Fundisho la Biblia?Mnara wa Mlinzi—2012 | Machi 1
-
-
a Kuungama kwamba Mungu ni mmoja kama inavyotajwa katika Shema, sala ambayo inategemea Kumbukumbu la Torati 6:4, ni sehemu muhimu ya ibada katika sinagogi.
-