Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nairobi—“Mahali Penye Maji Baridi”
    Amkeni!—2004 | Novemba 8
    • Jambo moja muhimu lililochangia ukuzi wa Nairobi ni ujenzi wa reli ya Kenya, ambayo wakati mmoja iliitwa Reli ya Kichaa.a Kufikia katikati ya mwaka wa 1899, kilometa 530 za reli hiyo zilikuwa zimekamilika, kuanzia jiji la pwani la Mombasa hadi Nairobi. Wakati huo, wajenzi wa reli hiyo walikuwa wametoka tu kushambuliwa na simba wawili ambao waliwaua wengi wa wafanyakazi wenzao, nao walikabili kazi ngumu ya kujenga reli katika eneo la Bonde Kuu la Ufa. Kwa kuwa reli hiyo ingefika ndani sana nchini, ilionekana kwamba mji wa Mombasa haukufaa tena kuwa sehemu kuu ya kuhifadhi bidhaa. Hata hivyo, ijapokuwa mandhari ya Nairobi haikupendeza, eneo hilo lilionwa kuwa linafaa kutumiwa kama kituo cha kupumzikia cha wafanyakazi na kituo cha kuhifadhia vifaa vya ujenzi. Mambo hayo yalichangia kufanya eneo hilo liwe jiji kuu la Kenya baadaye.

  • Nairobi—“Mahali Penye Maji Baridi”
    Amkeni!—2004 | Novemba 8
    • a Kwa habari kamili kuhusu ujenzi wa reli hiyo, ona makala “‘Reli ya Kichaa’ ya Afrika Mashariki,” katika gazeti la Amkeni! la Septemba 22, 1998, ukurasa wa 21-24.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki