Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Waridi Maridadi Kutoka Afrika
    Amkeni!—2007 | Oktoba
    • Waridi Maridadi Kutoka Afrika

      NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI KENYA

      “Ndiyo maua yenye kuvutia zaidi ambayo nimewahi kuona!” “Zawadi bora zaidi unayoweza kumpa rafiki mpendwa.” “Ni njia ya kusema, ‘Mtu fulani anakujali.’”

      HUENDA una maoni kama hayo yaliyoonyeshwa hapo juu ya wakazi wa Nairobi, Kenya.

  • Waridi Maridadi Kutoka Afrika
    Amkeni!—2007 | Oktoba
    • Kwa mfano, katika mwaka mmoja hivi karibuni zaidi ya asilimia 70 ya mamilioni ya maua yaliyosafirishwa kutoka nchini Kenya yalikuwa ya waridi na hivyo kuifanya Kenya kuwa moja ya nchi zinazokuza waridi zaidi ulimwenguni.

  • Waridi Maridadi Kutoka Afrika
    Amkeni!—2007 | Oktoba
    • Kutoka Shambani Hadi Nyumbani

      Watu wengi hununua waridi kutoka kwa wauzaji wa maua au dukani. Maua hayo hukuzwa katika mashamba makubwa na yanahitaji uangalifu mkubwa kuliko yale yanayopandwa katika bustani ya nyumbani. Tulipotembelea shamba moja karibu na Nairobi tuliona uangalifu wa ziada unaohitajika kutayarisha maua hayo ili yauzwe.

      Huko, kama katika maeneo mengine ya Kenya, mabanda ya kukuzia maua yanatambulisha shamba kubwa la kukuzia maua ya waridi. (Ona picha kwenye ukurasa wa 26.) Mabanda hayo hutumiwa kwa makusudi mengi. Maua ya waridi yaliyopandikizwa karibuni yanahitaji kulindwa kutokana na hali mbaya ya hewa. Mvua kubwa, upepo, au jua linapoyapiga moja wa moja linaweza kuyaharibu. Ili kudumisha hali sawa ya joto, ni muhimu kwamba hewa baridi iingizwe ndani ya mabanda hayo kwa urahisi na hewa yenye joto iondolewe.

      Ndani ya mabanda ya kukuzia maua hayo kuna mistari ya maua yaliyo katika hatua mbalimbali za ukuzi. Katika shamba hilo aina mbalimbali za waridi hukuzwa, kuanzia ua maarufu linaloitwa hybrid tea rose, lenye urefu wa sentimita 70 hivi, kufikia ua linaloitwa sweetheart rose lenye urefu wa sentimita 35 ambalo limezalishwa kutokana na waridi linaloitwa tea rose. Ekari mbili na nusu za shamba hilo zinaweza kuwa na mimea 70,000 hivi.

      Mimea hiyo hupataje virutubisho? Udongo wa kawaida hautumiwi. Maua hayo hukuzwa kwenye mawe ya volkano yaliyolazwa juu ya karatasi za plastiki. Hiyo ndiyo mbinu inayofaa zaidi kwani mawe hayo hayana magonjwa mengi yanayopatikana katika udongo. Mbinu fulani ya kunyunyizia maji hutumiwa ili kuipatia mimea maji. Katika mbinu hiyo, mabomba madogo yanaelekezwa kwenye maua na kutoa maji na virutubisho kwa kiwango kinachofaa. Udongo huo wa volkano una matundu madogo-madogo yanayoweza kuruhusu maji yapite, yakusanywe, na kutumiwa tena.

      Licha ya utunzaji wa hali ya juu unaotolewa, maua ya waridi yanaweza kuambukizwa magonjwa mbalimbali, hasa yale yanayosababishwa na kuvu. Yanatia ndani botrytis na ukungu, ambao huvamia majani na mashina ya mimea. Yasipochunguzwa, magonjwa hayo yanaweza kuathiri ubora wa maua. Kutumia dawa za kuua wadudu husaidia kudhibiti tatizo hilo.

      Wakati unapopita, rangi fulani nyangavu huanza kutokea, na hilo huonyesha wazi kwamba maua ya waridi yako tayari kuchumwa. Maua hayo hukatwa kwa uangalifu kabla matumba hayajafunguka. Wakati huo bado petali huwa hazijafunguka. Yanapochumwa wakati huo, hayanyauki upesi na vilevile rangi yake hudumu kwa muda mrefu. Hata hivyo, huenda wakati wa kuchumwa ukatofautiana kwa kutegemea aina ya ua. Ni muhimu kuchuma maua hayo asubuhi au jioni, wakati ambapo kuna unyevu na hayanyauki upesi. Maua yaliyochumwa hupelekwa kwenye chumba cha baridi ambako yanapunguzwa joto. Hilo pia huhakikisha kwamba maua hayo yanadumu kwa muda mrefu zaidi yakiwa yanapendeza.

      Baada ya hapo maua yatapitia hatua nyingine muhimu ya kupangwa. Katika hatua hii yatatenganishwa kulingana na rangi na ukubwa. Maua yanafungwa kulingana na matakwa ya mnunuzi. Mwishowe, maua yako tayari kuuzwa. Kutoka katika shamba hilo yanapelekwa hadi uwanja mkuu wa ndege jijini Nairobi, na kutoka hapo yatasafirishwa hadi Ulaya, umbali wa maelfu ya kilomita. Kwa sababu maua huharibika haraka, lazima yafikishwe sokoni ndani ya muda wa saa 24 baada ya kuvunwa, iwe soko hilo ni la karibu au la kimataifa.

      Kwa hiyo, wakati ujao ukipokea zawadi ya maua au ukiyanunua, tua ufikirie mwendo mrefu ambao yamesafiri, huenda hata ni ya Afrika. Labda hilo litakufanya umthamini zaidi Muumba, Yehova Mungu.—Zaburi 115:15.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki