-
Uzuri Mwingi Mno wa Kiti cha Ufalme cha Yehova cha KimbinguUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na kuzunguka kiti cha ufalme kuna viti vya ufalme ishirini na vinne, na juu ya viti vya ufalme hivi mimi niliona wameketi wazee ishirini na wanne wamevalia mavazi ya nje meupe, na juu ya vichwa vyao mataji ya dhahabu.” (Ufunuo 4:4, NW)
-
-
Uzuri Mwingi Mno wa Kiti cha Ufalme cha Yehova cha KimbinguUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Mtume Petro aliandikia Wakristo wapakwa-mafuta hivi: “Nyinyi ni ‘jamii iliyochaguliwa, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu kwa ajili ya mali ya pekee.’” (1 Petro 2:9, NW) Kwa kupendeza, ukuhani huo wa kale wa Kiyahudi, ulikuja kugawanywa ukawa migawanyo 24. Kila mgawanyo ulipewa mgawo wa majuma yao wenyewe katika mwaka wa kutumikia mbele za Yehova, hivi kwamba utumishi mtakatifu ulitolewa bila kukatizwa. (1 Nyakati 24:5-19) Basi, inafaa kwamba wako wazee 24 wakionyeshwa katika njozi ya Yohana ya ule ukuhani wa kimbingu kwa sababu huu ukuhani unatumikia Yehova kwa kuendelea, bila kukoma. Utakapokamilishwa, itakuwako migawanyo 24, kila mmoja ukiwa na washindi 6,000, kwa kuwa Ufunuo 14:1-4 hutuambia kwamba 144,000 (24 x 6,000) ‘wananunuliwa miongoni mwa aina ya binadamu’ wakasimame juu ya Mlima Sayuni wa kimbingu pamoja na Mwana-Kondoo, Yesu Kristo.
-