Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Pili cha Zaburi
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Juni 1
    • Zaburi ya 45 ni wimbo wa arusi ya mfalme na unabii kuhusu Mfalme wa Kimasihi.

  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Pili cha Zaburi
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Juni 1
    • 45:13, 14a—“Binti ya mfalme” ambaye “atapelekwa kwa mfalme” ni nani? Ni binti ya “Mfalme wa milele,” Yehova Mungu. (Ufunuo 15:3) Anawakilisha kutaniko lililotukuzwa la Wakristo 144,000, ambao Yehova amewafanya kuwa watoto wake kwa kuwatia mafuta kwa roho yake. (Waroma 8:16) “Binti” huyo wa Yehova ambaye ‘ametayarishwa kama bibi-arusi aliyepambwa kwa ajili ya mume wake,’ atapelekwa kwa bwana-arusi, yaani, Mfalme wa Kimasihi.—Ufunuo 21:2.

      45:14b, 15—“Mabikira” wanawakilisha nani? Wanawakilisha “umati mkubwa” wa waabudu wa kweli ambao wanajiunga na mabaki ya watiwa-mafuta na kuwasaidia. Kwa kuwa ‘wanatoka katika ile dhiki kuu’ wakiwa hai, watakuwa duniani wakati ndoa ya Mfalme wa Kimasihi itakapokamilishwa mbinguni. (Ufunuo 7:9, 13, 14) Wakati huo, watajawa na “furaha na shangwe.”

      45:16—Ni katika njia gani wana watachukua mahali pa mababu za mfalme? Yesu alipozaliwa duniani, alikuwa na mababu hapa duniani. Watakuwa wana wake atakapowafufua wakati wa Utawala wake wa Miaka Elfu. Baadhi yao watakuwa kati ya wale watakaowekwa kuwa “wakuu katika dunia yote.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki