-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
15. Ni wafalme gani wawili wenye nguvu waliotokana na falme nne za Kigiriki, nao walianzisha ushindani gani?
15 Kwa hiyo, wafalme wawili wenye nguvu—Niketa Seleuko wa Kwanza aliyetawala Siria na Ptolemy wa Kwanza aliyetawala Misri—waliibuka wakiwa wafalme wawili wenye nguvu kutokana na zile falme nne za Kigiriki. Ushindani wa muda mrefu unaofafanuliwa katika Danieli sura ya 11 kati ya “mfalme wa kaskazini” na “mfalme wa kusini,” ulianzishwa na wafalme hao wawili.
-
-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Seleuko alianzisha nasaba ya watawala wa Seleuko huko Siria. Miongoni mwa majiji aliyoanzisha mlikuwemo Antiokia—jiji kuu jipya la Siria—na bandari ya Seleucia. Baadaye mtume Paulo alifundisha huko Antiokia, ambapo wafuasi wa Yesu waliitwa Wakristo kwa mara ya kwanza. (Matendo 11:25, 26; 13:1-4) Seleuko aliuawa mwaka wa 281 K.W.K., lakini watawala wa nasaba yake waliendelea kutawala hadi mwaka wa 64 K.W.K. wakati ambapo Jenerali Mroma Gnaeus Pompey aliifanya Siria kuwa mkoa wa Roma.
-