Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wafalme Wawili Wapambana
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • 24. (a) Ni nini kilichompata Seleuko wa Tatu? (b) Mfalme Antiochus wa Tatu wa Siria ‘alifurika na kupita katikati’ ya milki ya mfalme wa kusini jinsi gani?

      24 Ni nini kilichotabiriwa kuhusu uzao wa Mfalme Seleuko wa Pili wa Siria? Malaika alimwambia Danieli hivi: “Na wanawe watafanya vita, na kukusanya mkutano wa majeshi makuu; watakaokuja na kufurika na kupita katikati; nao watarudi na kufanya vita mpaka penye ngome yake.” (Danieli 11:10) Na kabla ya miaka mitatu kutimia, utawala wa Seleuko wa Tatu ukakoma alipouawa. Ndugu yake, Antiochus wa Tatu, akatawala Siria baada yake. Mwana huyo wa Seleuko wa Pili alikusanya majeshi mengi ili akamshambulie mfalme wa kusini, ambaye wakati huo alikuwa Ptolemy wa Nne. Mfalme huyo mpya wa kaskazini wa Siria alipigana dhidi ya Misri na kukomboa bandari ya Seleucia, mkoa wa Coele-Siria, jiji la Tiro na jiji la Ptolemaïs, na miji ya karibu. Aliyashinda vibaya majeshi ya Mfalme Ptolemy wa Nne na kutwaa majiji mengi ya Yuda. Masika ya mwaka wa 217 K.W.K., Antiochus wa Tatu aliliacha Ptolemaïs na kwenda kaskazini, “mpaka penye ngome yake” huko Siria. Lakini punde si punde badiliko kubwa lingetokea.

  • Wafalme Wawili Wapambana
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • Mfalme wa Siria wa kaskazini, Antiochus wa Tatu, alikuwa ‘amepanga jeshi kubwa’ la watu 68,000 limkabili. Lakini “jeshi” hilo ‘liliwekwa mikononi’ mwa mfalme wa kusini katika pigano huko Raphia, jiji lililo pwani, karibu na mpaka wa Misri.

      26. (a) Ni “jeshi” gani lililochukuliwa na mfalme wa kusini katika pigano huko Raphia, na mkataba wa amani uliofanywa huko ulitia ndani nini? (b) Ni katika njia gani Ptolemy wa Nne ‘hakutumia wadhifa wake wenye nguvu’? (c) Mfalme wa kusini aliyefuata alikuwa nani?

      26 Unabii huo waendelea kusema hivi: “Atakapokwisha kuchukua lile jeshi, moyo wake utatukuzwa; naye atawaangusha makumi elfu; lakini hataongezewa nguvu [“hatatumia wadhifa wake wenye nguvu,” NW].” (Danieli 11:12) Ptolemy wa Nne, mfalme wa kusini, ‘alichukua’ askari 10,000 wa miguu na askari-wapanda-farasi 300 wa Siria akawaua na kutwaa wafungwa 4,000. Kisha wafalme hao wakafanya mkataba ambamo Antiochus wa Tatu aliachiwa Seleucia, bandari yake ya Siria lakini akapoteza Foinike na Coele-Siria.

  • Wafalme Wawili Wapambana
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • MPORAJI AREJEA

      27. Mfalme wa kaskazini alirudije “mwisho wa zamani zile” ili kukomboa eneo lililotekwa na Misri?

      27 Kwa sababu ya uporaji wake wote, Antiochus wa Tatu akaja kuitwa Antiochus Mkuu. Malaika alisema hivi juu yake: “Mfalme wa kaskazini atarudi, naye atapanga jeshi kubwa kuliko lile la kwanza; naye hakika atakuja mwisho wa zamani zile, yaani baada ya miaka kadha wa kadha, pamoja na jeshi kubwa na mali nyingi.” (Danieli 11:13) “Zamani zile” zilikuwa miaka 16 au zaidi baada ya Wamisri kuwashinda Wasiria huko Raphia. Mfalme Ptolemy wa Tano aliyekuwa mchanga alipotawazwa kuwa mfalme wa kusini, Antiochus wa Tatu alipanga “jeshi kubwa kuliko lile la kwanza” ili kukomboa maeneo yaliyokuwa yametwaliwa na mfalme wa kusini wa Misri. Ili kutekeleza lengo lake, alijiunga na Mfalme Philip wa Tano wa Makedonia.

  • Wafalme Wawili Wapambana
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • MPORAJI AREJEA

      27. Mfalme wa kaskazini alirudije “mwisho wa zamani zile” ili kukomboa eneo lililotekwa na Misri?

      27 Kwa sababu ya uporaji wake wote, Antiochus wa Tatu akaja kuitwa Antiochus Mkuu. Malaika alisema hivi juu yake: “Mfalme wa kaskazini atarudi, naye atapanga jeshi kubwa kuliko lile la kwanza; naye hakika atakuja mwisho wa zamani zile, yaani baada ya miaka kadha wa kadha, pamoja na jeshi kubwa na mali nyingi.” (Danieli 11:13) “Zamani zile” zilikuwa miaka 16 au zaidi baada ya Wamisri kuwashinda Wasiria huko Raphia. Mfalme Ptolemy wa Tano aliyekuwa mchanga alipotawazwa kuwa mfalme wa kusini, Antiochus wa Tatu alipanga “jeshi kubwa kuliko lile la kwanza” ili kukomboa maeneo yaliyokuwa yametwaliwa na mfalme wa kusini wa Misri. Ili kutekeleza lengo lake, alijiunga na Mfalme Philip wa Tano wa Makedonia.

      28. Mfalme mchanga wa kusini alikuwa na matatizo gani?

      28 Mfalme wa kusini alikuwa na matatizo pia ndani ya ufalme wake. “Zamani zile watu wengi watasimama ili kumpinga mfalme wa kusini,” malaika akasema. (Danieli 11:14a) Watu wengi “wa[li]simama ili kumpinga mfalme wa kusini.” Zaidi ya kukabili majeshi ya Antiochus wa Tatu na mwenzake Mmakedonia, mfalme huyo mchanga wa kusini alikuwa na matatizo nyumbani Misri. Kwa sababu mlezi wake Agathocles, aliyetawala akitumia jina lake, alikuwa akiwatenda vibaya Wamisri, wengi wao waliasi. Malaika aliongezea kusema hivi: “Wenye jeuri [“wana wa wapokonyaji,” NW] miongoni mwa watu wako watajiinua ili kuyathibitisha maono; lakini wataanguka.” (Danieli 11:14b) Hata baadhi ya watu wa Danieli walipata kuwa “wana wa wapokonyaji,” au wanamapinduzi. Lakini ‘ono’ lolote waliloona wanaume hao Wayahudi juu ya mwisho wa utawala wa wasio Wayahudi halikuwa la kweli, nao wangeshindwa, au ‘kuanguka.’

      29, 30. (a)“Silaha za kusini” zilishindwaje kukabiliana na shambulio kutoka kaskazini? (b) Mfalme wa kaskazini alipataje ‘kusimama katika nchi ya uzuri’?

      29 Malaika wa Yehova alitabiri hivi zaidi: “Mfalme wa kaskazini atakuja, na kufanya kilima [“atauzingira,” BHN], na kuupiga mji wenye maboma; na silaha za kusini hazitaweza kumpinga, wala watu wake wateule, wala hapatakuwa na nguvu za kumpinga. Maana ajaye kupigana naye atatenda kadiri apendavyo, walahapana mtu atakayesimama mbele yake; naye atasimama katika nchi ya uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi mwake.”—Danieli 11:15, 16.

      30 Majeshi ya Ptolemy wa Tano, au “silaha za kusini,” yalishindwa na shambulio kutoka kaskazini. Huko Paneas (Kaisaria Filipi), Antiochus wa Tatu alimfukuza Jenerali Scopas wa Misri pamoja na watu 10,000 aliochagua, au ‘wateule wake,’ hadi Sidoni, “mji wenye maboma.” Huko Antiochus wa Tatu ‘aliuzingira,’ na kuiteka bandari hiyo ya Foinike mwaka wa 198 K.W.K. Alitenda “kadiri apendavyo” kwa sababu majeshi ya mfalme wa kusini wa Misri hayakuweza kusimama mbele yake. Kisha Antiochus wa Tatu akapiga mwendo kuelekea Yerusalemu, jiji kuu la “nchi ya uzuri,” Yuda. Mwaka wa 198 K.W.K., Yerusalemu na Yuda ziliacha kutawalwa na mfalme wa kusini wa Misri na kuanza kutawalwa na mfalme wa kaskazini wa Siria. Naye Antiochus wa Tatu, mfalme wa kaskazini, akaanza ‘kusimama katika nchi ya uzuri.’ Mlikuwemo ‘uharibifu mikononi mwake’ kwa Wayahudi wote na Wamisri wote waliompinga. Mfalme huyo wa kaskazini angefanya apendavyo kwa muda mrefu kadiri gani?

      ROMA YAMZUIA MPORAJI

      31, 32. Kwa nini mfalme wa kaskazini hatimaye “a[li]fanya mapatano” ya amani na mfalme wa kusini?

      31 Malaika wa Yehova ajibu hivi: “Naye [mfalme wa kaskazini] atakaza uso wake ili aje pamoja na nguvu zote za ufalme wake, naye atafanya mapatano naye; naye atatenda kadiri apendavyo; naye atampa binti wa watu ili amharibu; lakini hilo halitasimama wala kumfaa [“naye hataendelea kuwa wake,” NW].”—Danieli 11:17.

      32 Mfalme wa kaskazini, Antiochus wa Tatu, ‘alikaza uso wake’ ili atawale Misri “pamoja na nguvu zote za ufalme wake.” Lakini hatimaye “alifanya mapatano” ya amani na Ptolemy wa Tano, mfalme wa kusini. Madai ya Roma yalikuwa yamemfanya Antiochus wa Tatu abadili mipango yake. Alipoungana na Mfalme Philip wa Tano wa Makedonia dhidi ya mfalme wa Misri mwenye umri mchanga ili watwae eneo lake, walezi wa Ptolemy wa Tano waliomba Roma iwalinde. Roma ilitwaa fursa hiyo ili kuongeza uvutano wake, ikaonyesha nguvu zake.

      33. (a) Ni masharti gani ya amani yaliyowekwa kati ya Antiochus wa Tatu na Ptolemy wa Tano? (b) Kusudi la ndoa kati ya Kleopatra wa Kwanza na Ptolemy wa Tano lilikuwa nini, na kwa nini mpango huo haukufua dafu?

      33 Akishurutishwa na Roma, Antiochus wa Tatu alimwekea masharti ya amani mfalme wa kusini. Badala ya kusalimisha maeneo aliyokuwa ameteka, kama vile Roma ilivyotaka, Antiochus wa Tatu alipanga kuyahamisha kwa jina tu kwa kumwoza binti yake Kleopatra wa Kwanza—“binti wa watu”—kwa Ptolemy wa Tano. Mikoa iliyotia ndani Yuda, “nchi ya uzuri,” ingetolewa ikiwa mahari. Hata hivyo, wakati wa ndoa mwaka wa 193 K.W.K. mfalme wa Siria hakuachilia mikoa hiyo imwendee Ptolemy wa Tano. Hiyo ilikuwa ndoa ya kisiasa, iliyofanywa ili kutiisha Misri chini ya Siria. Lakini, mpango huo haukufua dafu kwa sababu Kleopatra wa Kwanza ‘hakuendelea kuwa wake,’ kwa kuwa baadaye aliamua kumwunga mkono mume wake. Vita vilipozuka kati ya Antiochus wa Tatu na Waroma, Misri ilijiunga na Roma.

      34, 35. (a) Mfalme wa kaskazini aliuelekeza uso wake kwenye ‘nchi zipi za pwani’? (b) Roma ilikomeshaje “aibu” kutoka kwa mfalme wa kaskazini? (c) Antiochus wa Tatu alikufaje, na mfalme wa kaskazini aliyefuata alikuwa nani?

      34 Malaika alisema hivi akirejezea kushindwa huko kwa mfalme wa kaskazini: “Baada ya hayo [Antiochus wa Tatu] atauelekeza uso wake kwenye visiwa, naye atavipiga visiwa vingi [“nchi nyingi za pwani na kuzishinda,” BHN]; lakini mkuu mmoja [Roma] ataikomesha aibu iliyoletwa na yeye [Roma]; naam, aibu yake [kutoka kwa Antiochus wa Tatu] hiyo [Roma] atamrudishia mwenyewe. Ndipo [Antiochus wa Tatu] atauelekeza uso wake kwenye ngome za nchi yake mwenyewe; lakini atajikwaa na kuanguka, wala hataonekana tena.”—Danieli 11:18, 19.

      35 ‘Nchi hizo za pwani’ ni Makedonia, Ugiriki, na Asia Ndogo. Vita vilizuka Ugiriki mwaka wa 192 K.W.K., na Antiochus wa Tatu akashawishiwa aende Ugiriki. Hatimaye Roma ikatangaza vita dhidi yake kwa kuwa ilikasirishwa na jitihada za mfalme wa Siria za kuteka maeneo zaidi huko. Huko Thermopylae alishindwa na Waroma. Mwaka mmoja hivi baada ya kushindwa katika vita ya Magnesia mwaka wa 190 K.W.K., alilazimika kuacha kila kitu huko Ugiriki, Asia Ndogo, na maeneo yaliyo magharibi mwa Milima Taurus. Roma ilimtoza faini kubwa na kusitawisha utawala wake juu ya mfalme wa kaskazini wa Siria. Akiwa amefukuzwa kutoka Ugiriki na Asia Ndogo na baada ya kupoteza karibu meli zake zote, Antiochus wa Tatu ‘aliuelekeza uso wake mwenyewe kwenye ngome za nchi yake mwenyewe,’ Siria. Waroma walikuwa ‘wamemrudishia aibu yake mwenyewe.’ Antiochus wa Tatu alikufa akijaribu kupora hekalu huko Elymaïs, Uajemi, mwaka wa 187 K.W.K. Kwa hiyo, ‘akaanguka’ katika kifo naye mwana wake Seleuko wa Nne, akatawala baada yake akiwa mfalme wa kaskazini aliyefuata.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki