-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Badala yake, Ptolemy wa Nne alianza maisha ya ufasiki, na mwana wake mwenye umri wa miaka mitano, Ptolemy wa Tano, akawa mfalme wa kusini aliyefuata miaka kadhaa kabla ya kifo cha Antiochus wa Tatu.
-
-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
28. Mfalme mchanga wa kusini alikuwa na matatizo gani?
28 Mfalme wa kusini alikuwa na matatizo pia ndani ya ufalme wake. “Zamani zile watu wengi watasimama ili kumpinga mfalme wa kusini,” malaika akasema. (Danieli 11:14a) Watu wengi “wa[li]simama ili kumpinga mfalme wa kusini.” Zaidi ya kukabili majeshi ya Antiochus wa Tatu na mwenzake Mmakedonia, mfalme huyo mchanga wa kusini alikuwa na matatizo nyumbani Misri. Kwa sababu mlezi wake Agathocles, aliyetawala akitumia jina lake, alikuwa akiwatenda vibaya Wamisri, wengi wao waliasi.
-
-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
na silaha za kusini hazitaweza kumpinga, wala watu wake wateule, wala hapatakuwa na nguvu za kumpinga.
-
-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
30 Majeshi ya Ptolemy wa Tano, au “silaha za kusini,” yalishindwa na shambulio kutoka kaskazini. Huko Paneas (Kaisaria Filipi), Antiochus wa Tatu alimfukuza Jenerali Scopas wa Misri pamoja na watu 10,000 aliochagua, au ‘wateule wake,’ hadi Sidoni, “mji wenye maboma.” Huko Antiochus wa Tatu ‘aliuzingira,’ na kuiteka bandari hiyo ya Foinike mwaka wa 198 K.W.K.
-
-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
32 Mfalme wa kaskazini, Antiochus wa Tatu, ‘alikaza uso wake’ ili atawale Misri “pamoja na nguvu zote za ufalme wake.” Lakini hatimaye “alifanya mapatano” ya amani na Ptolemy wa Tano, mfalme wa kusini. Madai ya Roma yalikuwa yamemfanya Antiochus wa Tatu abadili mipango yake. Alipoungana na Mfalme Philip wa Tano wa Makedonia dhidi ya mfalme wa Misri mwenye umri mchanga ili watwae eneo lake, walezi wa Ptolemy wa Tano waliomba Roma iwalinde. Roma ilitwaa fursa hiyo ili kuongeza uvutano wake, ikaonyesha nguvu zake.
33. (a) Ni masharti gani ya amani yaliyowekwa kati ya Antiochus wa Tatu na Ptolemy wa Tano? (b) Kusudi la ndoa kati ya Kleopatra wa Kwanza na Ptolemy wa Tano lilikuwa nini, na kwa nini mpango huo haukufua dafu?
33 Akishurutishwa na Roma, Antiochus wa Tatu alimwekea masharti ya amani mfalme wa kusini. Badala ya kusalimisha maeneo aliyokuwa ameteka, kama vile Roma ilivyotaka, Antiochus wa Tatu alipanga kuyahamisha kwa jina tu kwa kumwoza binti yake Kleopatra wa Kwanza—“binti wa watu”—kwa Ptolemy wa Tano. Mikoa iliyotia ndani Yuda, “nchi ya uzuri,” ingetolewa ikiwa mahari. Hata hivyo, wakati wa ndoa mwaka wa 193 K.W.K. mfalme wa Siria hakuachilia mikoa hiyo imwendee Ptolemy wa Tano. Hiyo ilikuwa ndoa ya kisiasa, iliyofanywa ili kutiisha Misri chini ya Siria. Lakini, mpango huo haukufua dafu kwa sababu Kleopatra wa Kwanza ‘hakuendelea kuwa wake,’ kwa kuwa baadaye aliamua kumwunga mkono mume wake. Vita vilipozuka kati ya Antiochus wa Tatu na Waroma, Misri ilijiunga na Roma.
-
-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
36. (a) Mfalme wa kusini alijaribu kuendelezaje pambano, lakini akapatwa na nini? (b) Seleuko wa Nne aliangukaje, na ni nani aliyetawala baada yake?
36 Akiwa mfalme wa kusini, Ptolemy wa Tano alijaribu kuipata mikoa ambayo alipaswa kupewa ikiwa mahari ya Kleopatra, lakini alitiliwa sumu.
-