Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maisha Yenye Kuthawabisha Katika Utumishi wa Yehova
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Novemba 1
    • Nathan Knorr, aliyekuja Betheli akiwa na miaka 18 katika mwaka wa 1923, alikuwa msimamizi wa kiwanda katika miaka ya 1930. Alitembea kiwandani kila siku na kumsalimu kila mfanyakazi. Tulithamini sana upendezi huo wa kibinafsi hasa sisi tuliokuwa wapya Betheli. Katika mwaka wa 1936, tulipata matbaa mpya kutoka Ujerumani na kwa sababu baadhi ya ndugu vijana hawakuweza kuiunganisha, Ndugu Knorr alivaa ovaroli akafanya kazi pamoja nao kwa zaidi ya mwezi mmoja, hadi ilipoanza kufanya kazi.

      Ndugu Knorr alikuwa mfanyakazi mwenye bidii sana hivi kwamba wengi wetu hatungeweza kufanya kazi kama alivyofanya. Lakini alifurahia tafrija pia. Hata baada ya kuwekwa kuwa msimamizi wa kazi ya kuhubiri ulimwenguni pote ya Mashahidi wa Yehova katika Januari 1942, wakati mwingine alicheza besiboli na washiriki wa familia ya Betheli pamoja na wanafunzi wa shule ya wamishonari ya Gileadi katika chuo kimoja karibu na South Lansing, New York.

  • Maisha Yenye Kuthawabisha Katika Utumishi wa Yehova
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Novemba 1
    • Baada ya kifo chake mwaka wa 1942, Ndugu Knorr akachukua mahali pake na akafanya bidii kuwa msemaji bora hadharani. Kwa sababu chumba changu kilikuwa karibu na chake, mara nyingi nilimsikia akifanya mazoezi ya hotuba zake. Punde si punde ijapokuwa kwa juhudi nyingi, akawa msemaji bora.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki