Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Neno la Yehova Laendelea Kusonga Mbele Kasi (1976-1992)
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Lakini kufikia kiangazi cha 1976, N. H. Knorr mwenye umri wa miaka 71 alikuwa ameona kwamba alikuwa na mwelekeo wa kugonga vitu apitapo. Machunguzi yaliyofuliza yalionyesha kwamba alikuwa na uvimbe ubongoni usioweza kupasuliwa. Aling’ang’ana ili aendelee kubeba mzigo wa kazi kwa miezi fulani, lakini hakukuwa na matumaini kuwa afya yake ya kimwili ingepata nafuu.

  • Neno la Yehova Laendelea Kusonga Mbele Kasi (1976-1992)
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Katika vuli ya 1976, ujapokuwa uhakika wa kwamba hakukuwa na matumaini ya kuwa afya yake ya kimwili ingepata nafuu, Ndugu Knorr alishiriki kutoa maagizo yaliyotolewa kwenye mikutano iliyofanywa kwenye makao makuu pamoja na washiriki wa Halmashauri za Tawi na wafanyakazi wengine wa tawi kutoka ulimwenguni pote. Kuongezea kushiriki katika mikutano wakati wa mchana, Ndugu Knorr alialika ndugu hao kwenye chumba chake jioni wakiwa vikundi vidogovidogo. Kwa njia hiyo yeye na Audrey, mke wake, walikuwa na ushirika wa karibu na wanaume hao waliomjua na kumpenda na ambao alikuwa ameshughulika nao kwa ukaribu sana kwa miaka iliyopita. Kufuata mikutano hiyo, afya ya Ndugu Knorr ilizidi kudhoofika mpaka kifo chake Juni 8, 1977.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki