Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nimejionea Mabadiliko Makubwa Nchini Korea
    Amkeni!—2008 | Desemba
    • Nimejionea Mabadiliko Makubwa Nchini Korea

      Limesimuliwa na Chong-il Park

      “Mwoga! Unaogopa kufa vitani. Unajaribu kuepuka kuingia jeshini kwa kudai kwamba una sababu za kidini.” Hivyo ndivyo kapteni wa Shirika la Upelelezi la CIC alivyoniambia nilipokuwa mbele yake mnamo Juni (Mwezi wa 6) 1953, zaidi ya miaka 55 iliyopita.

      HILO lilitokea wakati wa Vita vya Korea. Kisha kapteni huyo akatoa bastola na kuiweka juu ya dawati. “Sasa, utakufa papa hapa badala ya kule vitani,” akasema. “Ungependa kubadilisha mawazo yako?”

      “Hapana,” nilijibu kwa uthabiti. Kwa hiyo, kapteni akamwamuru ofisa mmoja ajitayarishe kuniua.

      Nilijikuta katika hali hiyo kwa sababu nilikuwa nimeamriwa nitumike jeshini, lakini nikakataa. Tulipokuwa tukisubiri nilimwambia kapteni kwamba tayari nilikuwa nimeweka maisha yangu wakfu kwa Mungu, hivyo niliamini kwamba haingekuwa sawa kudhabihu maisha yangu kwa sababu nyingine yoyote isipokuwa kwa utumishi wa Mungu. Kisha dakika kadhaa zilipita huku tukiwa tumenyamaza. Muda mfupi baadaye, ofisa huyo alirudi na kusema kwamba kila kitu kilikuwa tayari kwa ajili ya kuuawa kwangu.

      Wakati huo, watu wengi huko Korea Kusini hawakujua mengi kuhusu Mashahidi wa Yehova. Pia hawakujua chochote kuhusu kukataa kwetu kushiriki katika mambo ya kijeshi ya serikali yoyote kwa sababu za kidini.

  • Nimejionea Mabadiliko Makubwa Nchini Korea
    Amkeni!—2008 | Desemba
    • Mnamo Januari 1953, nilifurahi kupokea barua iliyonialika kwenda kwenye Shule ya Gileadi huko New York ili nizoezwe kuwa mmishonari. Hata hivyo, baada ya kukata tikiti ya ndege, nilipata ujumbe kutoka kwa serikali ya Korea uliosema nijiunge na jeshi.

      Hali ya Kufa na Kupona

      Kwenye kituo cha kujiandikisha nilimweleza ofisa msimamo wangu wa kutounga mkono upande wowote katika mambo ya kisiasa na uamuzi wangu wa kutojiunga na jeshi. Kwa sababu hiyo, alinipeleka kwenye Shirika la Upelelezi la CIC ili wachunguze ikiwa mimi ni Mkomunisti. Hapo ndipo nilikabili hali ya kufa na kupona niliyotaja awali. Lakini badala ya kunipiga risasi, kapteni huyo alisimama ghafula, akampa ofisa mmoja ubao mnene, na akamwamuru anipige. Ingawa nilihisi uchungu mwingi, nilifurahi kwamba nilifaulu kuvumilia.

      Maofisa wa CIC walinirudisha kwenye kituo cha kujiandikisha ambako maofisa, wakipuuza imani yangu, walinipa namba ya utambulisho wa kijeshi bila kujali, na wakanipeleka kwenye kituo cha kijeshi kwenye kisiwa cha Cheju, karibu na Korea bara. Asubuhi iliyofuata, wote waliokuwa wametoka tu kuandikishwa kutia ndani mimi, walipaswa kula kiapo ili wawe wanajeshi. Nilikataa kufanya hivyo. Kwa sababu hiyo, nilishtakiwa katika mahakama ya kijeshi na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani.

      Maelfu Wadumisha Utimilifu

      Siku niliyopaswa kuondoka kwa ajili ya shule ya wamishonari, niliona ndege ikipaa angani. Ilikuwa ndege niliyostahili kusafiri nayo. Badala ya kuvunjika moyo kwa sababu singeweza kwenda Gileadi, niliridhika sana kwani nilikuwa nikidumisha utimilifu wangu kwa Yehova. Mimi si Shahidi pekee aliyekataa kutumika jeshini nchini Korea. Kwa kweli, Mashahidi zaidi ya 13,000 wamefanya vivyo hivyo katika miaka iliyofuata. Wametumika kwa jumla ya miaka zaidi ya 26,000 katika magereza nchini Korea.

  • Nimejionea Mabadiliko Makubwa Nchini Korea
    Amkeni!—2008 | Desemba
    • Mnamo 1953, niliposimamishwa mbele ya mahakama ya kijeshi, serikali ya Korea haikuelewa kwa nini mtu angekataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri. Baadhi yetu tulishtakiwa kuwa Wakomunisti, na Mashahidi wachache walipigwa mpaka wakafa. Wengi ambao walifungwa kwa sababu ya kukataa kuingia jeshini walipokuwa vijana wamewaona wana wao, na hata wajukuu wao, wakifungwa kwa sababu hiyohiyo.

      Kwa miaka michache iliyopita, vyombo vya habari vimeangazia visa vya Mashahidi wa Yehova wanaokataa kujiunga na jeshi la nchi yoyote kwa sababu ya dhamiri zao. Wakili mmoja aliyekuwa amemshtaki Shahidi fulani aliyekataa kujiunga na jeshi, aliandika barua ya kuomba msamaha ambayo ilichapishwa katika gazeti moja maarufu.

      Ninatumaini kwamba haki yetu ya kukataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri itaheshimiwa nchini Korea Kusini kama inavyoheshimiwa katika nchi nyingine nyingi. Ninasali kwamba serikali ya Korea Kusini haitawasumbua watu walio na imani kama yangu na kukomesha zoea la kuwafunga vijana wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri, “ili tuendelee kuishi maisha shwari na matulivu.”—1 Timotheo 2:1, 2.

  • Nimejionea Mabadiliko Makubwa Nchini Korea
    Amkeni!—2008 | Desemba
    • [Blabu katika ukurasa wa 14]

      Mashahidi Wakorea wamefungwa kwa jumla ya miaka 26,000 kwa kukataa kuingia jeshini

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki