-
Sehemu ya 3—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Wakati Ndugu Knorr na Ndugu Franz walipokuwa wakifanya safari hizo za utumishi, wamishonari zaidi waliozoezwa Gileadi walikuwa wakiwasili katika migawo yao. Kufikia mwisho wa 1944, baadhi yao walikuwa wakitumikia katika Kosta Rika, Mexico, na Puerto Riko. Katika 1945, wamishonari wengine walikuwa wakisaidia kupanga kitengenezo vizuri zaidi kazi ya kuhubiri katika Barbados, Brazili, Honduras ya Uingereza (sasa ni Belize), Chile, Kolombia, El Salvador, Guatemala, Haiti, Jamaika, Nikaragua, Panama, na Uruguai. Wakati wamishonari wawili wa kwanza walipowasili katika Jamhuri ya Dominika katika 1945, walikuwa ndio Mashahidi pekee katika nchi hiyo. Matokeo ya huduma ya wamishonari hao wa mapema yalihisiwa upesi. Trinidad Paniagua alisema hivi kuhusu wamishonari wa kwanza waliotumwa Guatemala: “Hilo ndilo tulilohitaji hasa—walimu wa Neno la Mungu ambao wangetusaidia kuelewa jinsi ya kufanya kazi.”
-
-
Sehemu ya 3—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Ramani/Picha katika ukurasa wa 460]
Kufikia mwishoni-mwishoni mwa 1945, wamishonari kutoka Shule ya Gileadi walikuwa tayari wameanza utumishi katika nchi 18 katika sehemu hii ya ulimwengu
Charles na Lorene Eisenhower
Kuba
John na Adda Parker
Guatemala
Emil Van Daalen
Puerto Riko
Olaf Olson
Kolombia
Don Burt
Kosta Rika
Gladys Wilson
El Salvador
Hazel Burford
Panama
Louise Stubbs
Chile
-