-
Je, Una “Akili ya Kristo”?Mnara wa Mlinzi—2000 | Februari 15
-
-
1. Yesu aonyeshwaje katika michoro mingi ya Jumuiya ya Wakristo, na kwa nini hiyo si picha ifaayo ya Yesu?
“HAJAWAHI kuonekana akicheka.” Hivyo ndivyo Yesu anavyosemwa katika hati moja inayodai kwa uwongo kuwa iliandikwa na ofisa mmoja wa kale wa Roma. Inasemekana kwamba hati hiyo, ambayo imejulikana kuwa imedumu ikiwa katika hali hiyo tangu karne ya 11, imeshawishi wachoraji wengi.a Katika michoro kadhaa, Yesu aonekana kama mtu mwenye huzuni ambaye hatabasamu hata kidogo. Lakini hiyo si picha ifaayo ya Yesu, ambaye anaonyeshwa katika Gospeli akiwa mtu mchangamfu, mwenye fadhili na hisia za ndani.
-
-
Je, Una “Akili ya Kristo”?Mnara wa Mlinzi—2000 | Februari 15
-
-
Je, si jambo muhimu kwamba hata watoto walistarehe wakiwa naye? Hakika hawangeweza kuvutiwa na mtu asiye mchangamfu, asiye na furaha na ambaye hatabasamu wala kucheka kamwe!
-