Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ulimwengu Mzima Waharibiwa!
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Machi 1
    • Uthibitisho mwingine kwamba kulikuwa na Gharika wapatikana katika mapokeo ya wanadamu. Karibu watu wote wa kale wana hekaya zinazosema kwamba wazazi wao wa kale waliokoka furiko la ulimwenguni pote. Mbilikimo wa Afrika, Wainka wa Marekani, Waselti wa Ulaya—wote wana hekaya zinazofanana na za watu wa Alaska, Amerika Kaskazini, Australia, China, India, Lithuania, Mexico, Micronesia, na New Zealand, kwa kutaja nchi chache tu.

      Bila shaka, kadiri wakati ulivyopita ndivyo hekaya hizo zilivyotiwa chumvi, lakini zote zina mambo kadhaa yanayoonyesha kwamba zilikuwa na chanzo kimoja: Mungu alichukizwa na uovu wa wanadamu. Akaleta furiko kubwa lililoangamiza wanadamu wote isipokuwa wachache tu waliokuwa waadilifu. Wanadamu hao waadilifu walijenga meli ambayo ilitumiwa kuwaokoa na kuokoa wanyama pia. Baadaye, ndege walitumwa kutafuta nchi kavu. Hatimaye meli ilitua juu ya mlima. Waliposhuka kutoka katika meli hiyo, waokokaji hao walitoa dhabihu.

      Jambo hilo linathibitisha nini? Haiwezekani mambo hayo yanayofanana yawe yalitokea tu. Hekaya hizo zote zinathibitisha ushuhuda wa kale wa Biblia kwamba wanadamu wote ni wazao wa waokokaji wa furiko lililoangamiza wanadamu. Hivyo, hatuhitaji kutegemea hekaya au ngano kujua yaliyotokea. Tuna Maandiko ya Kiebrania ya Biblia yaliyohifadhiwa vizuri.—Mwanzo, sura ya 6-8.

  • Ulimwengu Mzima Waharibiwa!
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Machi 1
    • [Chati katika ukurasa wa 4]

      Hekaya za Ulimwenguni Pote Kuhusu Lile Furiko

      Nchi Waleta Habari 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10

      Ugiriki 7 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      Roma 6 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      Lithuania 6 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      Ashuru 9 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      Tanzania 7 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      India - Hindu 6 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      New Zealand - Maori 5 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      Micronesia 7 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      Washington Marekani - Yakima 7 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      Mississippi Marekani - Choctaw 7 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      Mexico - Michoacan 5 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      Amerika Kusini - Quechua 4 ◆ ◆ ◆ ◆

      Bolivia - Chiriguano 5 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      Guyana - Arawak 6 ◆ ◆ ◆ ◆ ◆ ◆

      1: Mungu akasirishwa na uovu

      2: Uharibifu kupitia furiko

      3: Kwa agizo la Mungu

      4: Mungu atoa onyo

      5: Wanadamu wachache waokoka

      6: Waokolewa katika meli

      7: Wanyama waokolewa

      8: Ndege au kiumbe mwingine atumwa nje

      9: Hatimaye meli yatua juu ya mlima

      10: Dhabihu yatolewa

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki