-
Usahihi wa Biblia Unathibitishwa na Maktaba ya Kale ya UrusiMnara wa Mlinzi—2005 | Julai 15
-
-
Firkovich alikusanya hati nyingi sana na mwaka wa 1859 akaamua kuiuzia Maktaba ya Milki hati hizo. Mwaka wa 1862, Aleksanda wa Pili alisaidia kununua hati hizo kwa ajili ya maktaba hiyo kwa gharama kubwa sana, yaani rubo 125,000. Wakati huo gharama ya kuendesha maktaba hiyo haikuzidi rubo 10,000 kwa mwaka! Kodeksi ya Leningrad (B 19A) inayojulikana sana ilikuwa kati ya hati hizo zilizonunuliwa. Hati hiyo iliyoandikwa mwaka wa 1008 hivi ni nakala ya kale zaidi ya Maandiko yote ya Kiebrania. Msomi mmoja alisema kwamba “huenda hiyo ndiyo hati ya Biblia iliyo muhimu kuliko hati nyingine zote kwa sababu chapa nyingi za kisasa za Biblia ya Kiebrania zenye nyongeza zinategemea hati hiyo.” (Ona sanduku.)
-
-
Usahihi wa Biblia Unathibitishwa na Maktaba ya Kale ya UrusiMnara wa Mlinzi—2005 | Julai 15
-
-
Kwa mfano, Biblia Hebraica Stuttgartensia na Biblia Hebraica ya Kittel ambazo zilitumiwa na Halmashauri ya Kutafsiri Biblia ya Ulimwengu Mpya zinategemea Kodeksi ya Leningrad inayotaja jina la Mungu mara 6,828 katika maandishi ya awali.
-