-
Kwa Nini Unaweza Kuamini Vitabu vya Injili vya Biblia?Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 1
-
-
Namna gani dai la kwamba vitabu vya Injili vya Biblia vilibadilishwa ili kuficha masimulizi fulani ya maisha ya Yesu? Kwa mfano, je, kuna uthibitisho wowote kwamba Injili ya Yohana ilibadilishwa katika karne ya nne ili kupotosha ukweli? Ili kujibu swali hilo, tunahitaji kukumbuka kwamba chanzo kimoja kikuu cha Biblia ya leo ni hati ya karne ya nne inayoitwa Vatican 1209. Ikiwa Biblia yetu ina mabadiliko yaliyofanywa katika karne ya nne, basi mabadiliko hayo yangekuwa katika hati hiyo. Jambo la kufurahisha ni kwamba hati nyingine ambayo ina sehemu kubwa ya kitabu cha Luka na Yohana, inayoitwa Bodmer 14, 15 (P75), iliandikwa kati ya mwaka wa 175 W.K. na 225 W.K. Wataalamu wanasema kwamba maandishi yake yanalingana sana na yale ya Vatican 1209. Yaani, hakuna mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika vitabu vya Injili vya Biblia, na hati ya Vatican 1209 inathibitisha hilo.
-
-
Kwa Nini Unaweza Kuamini Vitabu vya Injili vya Biblia?Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 10]
Vatican 1209
Hati ya karne ya nne ya Vatican 1209, iliyo hapo juu, inaonyesha kwamba maandishi ya Injili hayakubadilika sana
[Hisani]
From the book Bibliorum Sacrorum Graecus Codex Vaticanus, 1868
-