-
‘Midomo ya Kweli Itathibitishwa Milele’Mnara wa Mlinzi—2003 | Machi 15
-
-
‘Kosa Linalotia Mtu Mtegoni’
Sulemani anasema, “Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya; bali mwenye haki atatoka katika taabu.” (Mithali 12:13) Kusema uongo ni dhambi ya midomo ambayo inaweza kuwa kama mtego wenye kuua kwa wale wanaouzoea. (Ufunuo 21:8) Kusema uongo kunaweza kuonekana kama njia rahisi ya kuepuka adhabu au hali mbaya. Mara nyingi mtu anaposema uongo analazimika kusema uongo tena. Kama vile mtu anayeanza kucheza kamari kwa pesa kidogo anavyoshawishika kutumia pesa nyingi zaidi akijaribu kuokoa zile alizopoteza, ndivyo mtu anayesema uongo hujikuta amenaswa katika mtego mbaya wa kusema uongo tena na tena.
Kosa la midomo humtia mtu mtegoni katika maana ya kwamba anayewadanganya wengine huishia kujidanganya mwenyewe. Kwa mfano, huenda mtu mwongo akafikiri kwamba anajua mengi na ni mwerevu sana, ilhali anajua machache sana. Hivyo basi anaanza kujidanganya. Kwa kweli, ‘yeye hujipendekeza machoni pake kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa.’ (Zaburi 36:2) Uongo unakuwa mtego ulioje! Kwa upande mwingine, mwadilifu hatajiingiza katika hali hiyo ngumu. Hata akipatwa na shida, hatadanganya.
-
-
‘Midomo ya Kweli Itathibitishwa Milele’Mnara wa Mlinzi—2003 | Machi 15
-
-
Kosa la midomo linaweza kusababisha madhara makubwa katika kikao cha hukumu. Mfalme wa Israeli anasema: “Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki; bali shahidi wa uongo hutamka hila.” (Mithali 12:17) Shahidi wa kweli hutamka ukweli kwa sababu ushuhuda wake unategemeka na ni wenye kuaminika. Maneno yake huchangia kutekelezwa kwa haki. Lakini, shahidi wa uongo hudanganya na huchangia kupotoshwa kwa haki.
-
-
‘Midomo ya Kweli Itathibitishwa Milele’Mnara wa Mlinzi—2003 | Machi 15
-
-
Mfalme mwenye hekima anasema, “Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu; bali wafanyao mashauri ya amani, kwao kuna furaha.” Mfalme huyo anaendelea kusema: “Mwenye haki hatapatikana na msiba wowote; bali wasio haki watajazwa mabaya.”—Mithali 12:20, 21.
Wanaopanga hila wanaweza tu kusababisha maumivu na mateso. Lakini, washauri wa amani wanapata uradhi kwa kufanya mambo yanayofaa. Pia wanafurahia matokeo mazuri ya kufanya hivyo. Jambo lililo muhimu zaidi ni kwamba wanapata kibali cha Mungu kwa kuwa “midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA; bali watendao uaminifu ndio furaha yake.”—Mithali 12:22.
-